top of page

Tafakuri

 

Imeandikwa na stafu wa ULY CLINIC

06.06.2021

​

Namna ya kufanya vema tafakuri

 

Tafakuri ni njia ya kufunza ufahamu wako kumakinikia au kuzingatia wazo, kitu au tendo.  Kuna aina nyingi za tafakuri, kila moja ina ujuzi wake wa namna ya kufanyika.  Makala hii imelenga kukufunza namna ya kuanza kufanya tafakuri.

​

Mara nyingi watu wanaoanza kufanya tafakuri ni vigumu sana kufanya kwa muda mrefu unaoridhisha kwa sababu mawazo mengi huja na kutoka na kuharibu utulivu. Kwa sababu hiyo, zipo njia mbalimbali ambazo zinarahisisha kukufanya uelekeze mawazo yako kwenye kitu kimoja tu unachokitaka. Njia nzuri na rahisi ya kufanya tafakuri ni kupelekea mawazo yote kwenye upumuaji wako. Na mfano wa aina mojawapo ya tafakuri ni tafakuri makinifu.

 

Tafakuri makinifu

 

Kumakinikia jambo humaanisha kuweka mawazo kwenye kitu kimoja au pointi moja tu katikati ya vitu vingi, hili linaweza fanikiwa baada ya kuweka mawazo kwenye pumzi, kurudia rudia sema neno moja au msemo, kushangaa moto wa mshumaa ukiwa umefumba macho, kuhesabu shanga zilizotungwa au rozali.

​

Kwa sababu kumakinikia jambo moja ni kugumu, mtu asiye mzoefu wa kufanya tafakuri atafanya kwa muda mfupi sana na kushindwa kuendelea kwenye hali ya kudhibiti ufahamu wake. Ni vema kuendelea kufanya siku hadi siku mpaka pale utakapoona muda wa tafakuri unakutosha.

​

Aina hii ya tafakuri inatakiwa kukufanya uwe na uwezo wa kuweka ufahamu wako kwenye kitu kimoja au point moja kila mara ufahamu wako unapohama kuwaza kitu kingine, hii itasaidia kuongeza umakini wako kwenye kitu kimoja tu.

 

Tafakuri zingatifu

 

 

Tafakuri zingativu inamfanya mfanyaji kuweka mawazo yote yanayomjia kwenye ufahamu wake. Madhumuni si kumfanya amezwe na mawazo au kuyahukumu, bali kumfanya atambue uwepo wa kila wazo moja kwenye ufahamu wake.

​

Ukifanya tafakuri zingatifu, utaona jinsi gani mawazo na hisia zako zinavyohama na baada ya muda utakuwa mwelewa zaidi wa tabia za binadamu kuhukumu mambo kwa haraka kuwa ni mema au mabaya Kufanya tafakuri hii inakufanya uwe na uwiano ndani yako ya kuhukumu mambo vema.

​

Baadhi ya walimu wanaotoa mafunzo ya tafakuri, hufunza kufanya tafakuri zote mbili kwa pamoja yaani tafakuri zingatifu na makinifu.

 

Njia zingine za tafakuri

 

Kuna njia nyingine nyingi za kufanya tafakuri, mfano tafakuri tembezi, tafakuri mazoezi n.k . soma zaidi kwenye Makala zingine ndani ya tovuti hii.

 

Faida za kufanya takakuri

 

Imeonekana kuwa, kufanya tafakuri huupa mwili utulivu, hata hivyo hili si dhumuni la moja kwa moja la kufanya ya tafakuri bali ni matokeo tu. Madhumuni halisi ya kufanya tafakuri kutokana na tamaduni za ki Budha ni ukombozi wa ufahamu kushikamana na vitu ambavyo haiwezi kudhibiti kama hali za nje au hisia kali za ndani ili kuleta uwiano wa ndani na amaniya moyo.

 

Matokeo mengine ya tafakuri ambayo si madhumuni ya moja kwa moja na hutokea kwa muda mfupi ni;

  • Kushuka kwa shinikizo la damu

  • Kuongezeka kwa mzunguko wa damu

  • Kupunguza mapigo ya moyo

  • Kupunguza upumuaji

  • Kupunguza wasiwasi

  • Kupunguza kiwango cha homoni za msongo (cortisol)

  • Hisia za kuwa una afya

  • Kupunguza msongo

 

Faida za muda mrefu za tafakuri

 

Tafiti nyingi zinaendelea kufanyika kuchunguza endapo faida za muda mfupi zinaweza kuwa endelevu kwa watu wanaofanya tafakuri, hata hivyo, taarifa kutoka kwa wagonjwa wanaofanya programu hii ya tafakuri wameonyesha kupata faida kama zilivyoonyesha hapo juu, haswa katika kudhibiti msongo wa mawazo, kupunguza shinikizo la damu na wasiwasi

​

Namna ya kufanya tafakuri kwa wanaoanza

​

  • Kaa chini au lala kwenye kitu laini kama ilivyo kwenye picha

  • Fumba macho, unaweza kutumia kitambaa n.k

  • Usifanye jitihada yoyote kudhibiti upumuaji wako

  • Weka mawazo yako wako kwenye upumuaji wako tu kwa kuhisi jinsi kifua chako kinavyoenda juu na chini na hewa inavyopita puani na kutoka.

  •  Endapo ufahamu wako unahamia kwenye vitu vingine, rudisha ifikirie kuhusu upumuaji wako

  • Fanya hivyo kwa kurudia rudia kwa jinsi siku zinavyoenda

 

Malezo ya ziada unapata wapi?

​

Endapo unataka maelezo ya ziada wasiliana nasi tutakupatia maelekezo zaidi na msaada wa kitaalamu.

​

Imeboreshwa 09.06.2021

​

Nenda kurasa ya mazoezi na chakula kwa kubofya hapa

​

Rejea za mada hii

​

  1. Unconscious-mind. https://www.simplypsychology.org/unconscious-mind.html. Imechukuliwa 06.06.2021

  2. Falun Gong & Health. https://falunaz.net/falun-gong-online-course-en-1. Imechukuliwa 06.06.2021

  3. 12 must-know meditation tips for beginners. https://www.insider.com/meditation-tips-for-beginners. Imechukuliwa 06.06.2021

  4. Meditation for beginers. https://www.headspace.com/meditation/meditation-for-beginners. Imechukuliwa 06.06.2021

  5. 9 Types of Meditation: Which One Is Right for You?. https://www.healthline.com/health/mental-health/types-of-meditation. Imechukuliwa 06.06.2021 

  6. Meditation. https://www.mayoclinic.org/tests-procedures/meditation/about/pac-20385120.Imechukuliwa 06.06.2021  

​

kupumua-kwa-ndani-ulyclinic
bottom of page