top of page

Mwandishi:

Dkt. Mangwella S, M.D

Mhariri:

Dkt. Adolf S, M.D

Jumatatu, 24 Julai 2023

Mimba ya miezi saba

Mimba ya miezi saba

Mimba ya miezi saba ni sawa na mimba ya wiki 25 hadi 28, katika kipindi hiki mabadiliko mbalimbali hutokea mwilini katika kila wiki. Makala hii imeelezea kuhusu mabadiliko yanayotokea katika lila wiki ya mimba ya miezi saba.


Mimba ya wiki ishirini na tano (25)

Macho huanza kufumbuka na uono kuimarika, mapafu huzalisha ute utakaomuwezesha kupumua baada ya kuzaliwa.


Nini hutokea kwa mtoto
 • Macho huanza kufumbuka na uono wake huimarika

 • Mapafu huzalisha ute utakaomuwezesha kupumua baada ya kuzaliwa

 • Mishipa midogo midogo ya damu huanza kutengenezwa kwenye ngozi


Nini hutokea kwa mama
 • Huendelea kupata dalili na mabadiliko mbali mbali kama kwenye wiki zilizopita


Mimba ya wiki ishirini na sita (26)

Mtoto huendelea kukua na kuongezeka uzito, kwa mtoto wa kiume korodani zake huwa tayari zimeshuka kuingia kwenye kifuko cha korodani.


Nini hutokea kwa mtoto
 • Mtoto huendelea kukua na kuongezeka uzito

 • Kwa mtoto wa kiume korodani huwa zimeshuka kikamilifu kufikia mahala zinapotakiwa kuwa kama ilivyo kwa mtu mzima

 • Na kwa mtoto wa kike mfumo wake wa ndani wa uzazi huendelea kuimarika zaidi


Nini hutokea kwa mama

Mama huendelea kuona dalili na viashiria mbali mbali kama ilivyo kea wiki zilizopita.


Mimba ya wiki ishirini na saba (27)

Wiki hii huashiria mwisho wa kipindi cha pili cha ujauzito ambapo mtoto huongezeka zaidi uzito na mwili wa mama huanza kujiandaa kwa ajili ya leba.


Nini hutokea kwa mtoto
 • Kuongezeka uzito

 • Mifumo na ogani zake huwa zimekomaa kiasi kwamba kuna uwezekano wa kuishi endapo atazaliwa katika kipindi hiki


Nini hutokea kwa mama

Maudhi na dalili ambazo mama huziona katika kipindi hiki ni kutokana na kuongezeka kwa uzito wa mtoto na mji wa uzazi kutanuka sana, ambazo ni;

 • Kushindwa kupumua vizuri

 • Matatizo ya kupata usingizi

 • Kuvimba miguu, mikono au uso nk


Mimba ya wiki ishirini na nane (28)

Wiki hii ni mwanzo wa kipindi cha tatu cha ujauzito, mtoto huwa na mabadiliko makubwa kwenye ubongo na kutanguliza kichwa.


Nini hutokea kwa mtoto
 • Huwa na urefu wa takribani sentimeta 37 na uzito wa gramu 1000

 • Mabadiliko makubwa hutokea katika ubongo wake ili kufanania ubongo wa mtu mzima

 • Huanza kupata ndoto, kukapua macho na kuonesha hisia tofauti tofauti kama vile tabasamu nk

 • Huanza kugeuka, asilimia kubwa ya vichanga hutanguliza kichwa


Nini hutokea kwa mama

Pamoja na mabadiliko ambayo huanza wiki ya 27, kitu cha pekee ambacho huanza kuonekana katika wiki hii ni kuhisi maumivu ambayo hutaka kufanana na uchungu (braxton-Hicks contractions), (kusoma zaidi kuhusu dalili za uchungubofay hapa


Hali hii husababishwa na kutanuka na kusinyaa kwa misuli ya mji wa uzazi ambako huchukua muda wa sekunde 30 hadi dakika 2. Maumivu haya huwa hayana muendelezo na huwa ya kawaida japo huwa makali leba inapokaribia.

Imeboreshwa:

Jumatatu, 24 Julai 2023 20:30:05 UTC

Rejea za mada hii:

 1. American Society for Reproductive Medicine; American College of Obstetricians and Gynecologists' Committee on Gynecologic Practice. Prepregnancy counseling: Committee Opinion No. 762. Fertil Steril. 2019 Jan;111(1):32-42. [PubMed]

 2. Berglund A, et al. Preconception health and care (PHC)-a strategy for improved maternal and child health. Ups J Med Sci. 2016 Nov;121(4):216-221. [PMC free article] [PubMed]

 3. Annadurai K, et al. Preconception care: A pragmatic approach for planned pregnancy. J Res Med Sci. 2017;22:26. [PMC free article] [PubMed]

 4. McClatchey T, et al. Missed opportunities: unidentified genetic risk factors in prenatal care. Prenat Diagn. 2018 Jan;38(1):75-79. [PubMed]

 5. Ko SC, et al. Estimated Annual Perinatal Hepatitis B Virus Infections in the United States, 2000-2009. J Pediatric Infect Dis Soc. 2016 Jun;5(2):114-21. [PubMed]

 6. Tohme RA, et al. Hepatitis B virus infection among pregnant women in Haiti: A cross-sectional serosurvey. J Clin Virol. 2016 Mar;76:66-71. [PMC free article] [PubMed]

 7. Bhavadharini B, et al. Screening and diagnosis of gestational diabetes mellitus - relevance to low and middle income countries. Clin Diabetes Endocrinol. 2016;2:13. [PMC free article] [PubMed]

 8. ACOG Practice Bulletin No. 190 Summary: Gestational Diabetes Mellitus. Obstet Gynecol. 2018 Feb;131(2):406-408. [PubMed]

 9. Rule T, et al. Introducing a new collaborative prenatal clinic model. Int J Gynaecol Obstet. 2019 Mar;144(3):248-251. [PubMed]

bottom of page