top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

Dkt. Benjamin S, MD

Dkt. Lugonda, MD

7 Aprili 2026, 00:48:05

Kipandikizi

Kipandikizi kinachowekwa chini ya ngozi kuzuia mimba vinaweza kuwa vya aina tofauti, aina hizi hutegemea homoni zilizowekwa kwenye vipandikizi hivyo, kuna aina mbili za homoni zinazowekwa kwenye vipandikiza ikiwemo homoni ya estrojni na projesteroni

Kipandikizi kinaweza kuwa kilicho tengenezwa na estrojeni tu, kilicho tengenezwa na projesteroni tu au cha mchanganyiko wa projesteroni na estrogen. Kila aina ya kipandikizi kina kazi faida na madhara yake kwenye mwili wa binadamu

Sehemu hii tuzazungumzia aina hizi tofauti, kwanini unatumia aina Fulani, maudhi yanayoweza kutokea na namna ya kukabiliana nayo

Kipandikizi cha projesteroni tu

Kipandikizi hiki huwekwa chini ya ngozi, sehemu ya ndani ya mkono chini kidogo ya kwapa kwa ajili ya kuzuia mimba kwa mda mrefu. Kipandikizi hiki kinaweza kuwa na majina aina tofauti ya kibiashara kama implanon na nexplanon lakini vyote huwa na uwezo mzuri wa kuzuia mimba

Nani anatakiwa kutumia kipandikizi hiki?

Kipandikizi cha projesteroni tu huweza kutumiwa na wanawake wengi, kuna baadhi ya magonjwa au hali huweza kumzuia mwanamke kutumia vipandikizi hiki mfano mwanamke mwenye saratani ya titi/chuchu, na mwanamke mwenye ugonjwa wa ini. Shirika la afya ulimwenguni limeweka utaratibu wa mwanamke yupi atumie vipandikizi vya projesteroni tu.

Wanawake ambao wana hatari ya kupata mimba zisizotarajiwa, ikiwa pamoja na wasichana wadogo, wanawake waliotokwa na mimba, ni wanachama wa kutumia aina hii ya kipandikizi kwa sababu wanahatari ya kuacha matumizi ya njia zingine za uzazi wa mpango. Kwa tafiti zilizofanyika imeonyesha kwamba wanawake chini ya umri wa miaka 20 wanapenda njia hii za uzazi wa mpango zinazoweza kuzuia mimba kwa mda mrefu.

Nani hatakiwi tumia njia hii ya kipandikizi?

  • Mwanamke mwenye mimba au au anayeshukiwa kuwa anamimba

  • Hitoria iliyopita au ya sasa ya kuganda kwa damu

  • Kuwa na Saratani ya ini au ugonjwa wa ini

  • Kutokwa na damu kwenye via vya uzazi

  • Kujulikana au kuhisiwa kuwa na saratani ya matiti

  • Mzio/aleji kwenye homoni hii

Kwa wanawake waliopata au walio na tatizo la damu kuganda wanatakiwa kutumia kipandikizi chenye homon imchanganyiko wa estrojen na projesteroni.


Hufanyaje kazi kuzuia mimba?

Homoni ya projesteroni hubadili mazingira ya kwenye uke, kwa kubadilisha ute usiwe rafiki kwa mbegu za kiume kupita, pia huweza kuzuia mayai kuzalishwa kutoka kwenye ovary endapo dozi kubwa itatumika. Ingawa homoni ya projesteroni huzuia ukuta wa mimba kutokuwa rafiki kwa ajili ya kujipandikiza kwa mimba endapo mimba imetungishwa, kazi kubwa inayofanya ni kuzuia kutungishwa kwa mimba.

Muda wa kufanya kazi?

Kipandikizi hufanya kazi kulingana na muda ambao dawa iliyopo ndani yake itaisha, kuna vinavyofanya kazi kwa miaka mitatu. hadi mitano.

Maudhi au madhara yanayoweza kutokea kutokana na kipandikizi ni yapi?

Mzio. Kwa baadhi ya wanawake wenye aleji/mzio na homoni hii kwenye ngozi, wakiwekewa kipandikizi chini ya ngozi, ngozi zao hutengeneza wekundu, uvimbe, kuvilia kwa damu chini ya ngozi, na maumivu

Maudhi mengine ni kama maumivu, kutokwa damu kidogo, kuwashwa, kupata makovu wakati wa kuweka au kutoa kipandikizi.

Kubadilika kwa hedhi:

Wanawake wanaotumia vipandikizi wanaweza kuwa na kipindi kirefu au kifupi cha hedhi au kutotokwa na damu kabisa (amenorea). Maudhi makuu yanayotokea, kutokana na matumizi ya kipandikizi cha projesteroni tu huwa ni pamoja na, kutokwa na damu kwa kushitukiza, kutokwa na damu katikati ya mwezi ambapo hali hii inaweza isiishe au kupungua endapo mwanamke ataendelea kutumia kipandikizi hicho. Dalili hizi zimelipotiiwa na asilimia 11 ya watumiaji wa njia hii.

Kuvurugika kwa mpangilio wa hedhi hutokea sana mwanzoni wa matumizi ya kipandikizi haswa katika miezi mitatu ya mwaka wa kwanza tangu kuwekewa kwa kipandikizi, kisha kutoweka na kuamka tena mwaka wa pili na watatu wa matumizi. Wanawake waliopata kutokwa na damu mara kwa mara wengi walisimama/acha kuendelea kutumia njia hii.

Matibabu ya kutokwa na damu bila mpangilio si lazima, lakini kwa sababu kutokwa na damu husababisha mtumiaji kuona aache kutumia njia hiyo basi kuna njia za kuchukua ili kukabili tatizo hili. Njia hizo ni matumizi ya dawa za mda mfupi jamii ya NSAIDs,, matumizi ya dawa za kunywa zenye mchanganyiko wa homoni zote mbili, au kupewa homoni nyongeza ya estrojeni.

Kujua Matibabu ya kutokwa na damu nyingi kusikotkubalika ongea na daktari wako.

Madhara katika Mifupa

Kipandikizi cha projesteroni tu haipelekei mifupa kupoteza uimara wake kwa kasi sana ukilinganisha na njia ya sindano ya depo

Kipandikizi chenye homoni ya estrogeni hupunguza kiwango cha homoni ya insulin kwenye damu inayochakatua sukari mwilini, pia hupunguza kiwango cha lehemu aina ya HDL na LDL. Madhara ya upungufu huu yameonekana kwa wanawake waliotumia kitanzi cha projesteroni tu chini ya ngozi kwa mda wa miaka mitatu.

Maudhi mengineyo

Maudhi mengineyo ni kama maumivu ya kichwa, kuongezeka kwa uzito, maumivu ya matiti, mabadiliko ya hisia, maumivu ya tumbo. Wanawake njia za uzazi wa mpango zenye projesteroni huongezeka uzito wa kilo tatu katika miezi 36 ya matumizi ya njia husika.

Imeandikwa:

3 Novemba 2021, 12:31:24

ULY clinic inakushauri siku zote ufuate ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia mawasiliano yetu.

Rejea za mada:

bottom of page