Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
WAMJW
ULY CLINIC
24 Agosti 2026, 03:43:15

Chanjo ya COVID ni mpango wa kupunguza watu duniani?
Hakuna ushahidi!
Lengo kubwa la chanjo, ikiwa ni pamoja na hizi chanjo za COVID-19 ni kumkinga mtu aliepatiwa chanjo ama asipate maambukizi au asipate madhara makubwa au kumkinga na kifo kitokanacho na ugonjwa husika.
Ndio maana faida kubwa ya chanjo ya COVID-19 ni kumkinga mtu asipate COVID-19 kali au kumkinga na kifo kitokanacho na COVID-19. Hivyo basi hakuna ushahidi wowote wa kisayansi wa chanjo zilizopo ikiwa ni pamoja na chanjo ya COVID-19 kuathiri kwa namna yoyote ile mfumo wa via vya uzazi au kupunguza idadi ya watu. Na ndio maana tangu utotoni tumekuwa tumepata chanjo mbalimbali ikiwa ni pamoja na chanjo za Kifua kikuu, polio, surua, pepopunda na kadhalika, lakini hazijawahi kuathiri uweze wa watu kuzaa. Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ilichunguza chanjo hizi na kujiridhisha pasipo shaka kuwa hakuna kitu chochote ndani ya chanjo kinachoweza kuathiri mfumo wa uzazi.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:07:13
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
​
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
