Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
ULY CLINIC
24 Agosti 2026, 03:43:15
Mzio maana yake nini yaa tafsiri?
Mzio (aleji) ni hali ambapo mwili unakuwa na mwitikio mkali au usio wa kawaida kwa kitu fulani ambacho kwa kawaida hakisababishi madhara kwa watu wengi.
Kwa maneno rahisi, mzigo hutokea pale mfumo wa kinga unapokiona kitu fulani kama hatari na kuanza kupambana nacho, hata kama kitu hicho si hatari kwa mwili.
Vitu vinavyoweza kusababisha mzio ni pamoja na:
Vumbi
Vyakula fulani (kama mayai, karanga au dagaa)
Dawa baadhi
Harufu kali au kemikali
Manyoya ya wanyama
Poleni kutoka kwenye mimea
Dalili za mzio zinaweza kuwa:
Kupiga chafya mara kwa mara
Mafua au kuziba kwa pua
Kuwasha ngozi au macho
Vipele au upele kwenye ngozi
Kuvimba sehemu za mwili
Kwa hiyo, mzigo au aleji ni mwitikio wa kinga ya mwili dhidi ya kitu kinachochukuliwa kama kichocheo cha mzio (viasha mzio).
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 17:08:31
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
​
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:

