Imeandikwa na daktari wa ulyclinic
Afezia
Ni neno la Kiswahili lililotokanana neno la kiingereza aphasia lililotoka kwenye neno la kigiriki aphatos lenye maana kutoweza kuongea. Hivyo neno afezia linamaanisha kupoteza uwezo wa kuongea.
Afezia ni tatizo la lugha linaloathiri uwezo wa kuongea, kuelewa lugha pamoja na uwezo wa kusoma na kuandika. Hutokana na kuharibika kwa sehemu ya ubongo wa kushoto inayoitwa cerebro hemisphea, kuharibika huko kunakosababishwa na kiharusi, jeraha au uvimbe ndani ya kichwa.
Dalili zingine zinazoweza kuambatana ni zile za matatizo ya kuongea kama vile
disathria, na apraksia ya kuongea ambayo hutokana na majeruhi ndani ya ubongo.
Muulize daktari wako endapo una dalili hii kwa ushauri, uchunguzi na tiba
Imeboreshwa 10.03.2020
Rejea
-
Ulyclinic
-
Oxford English dictionary