top of page

Imeandikwa na Daktari wa ulyclinic

Kupoteza nywele mwilini-Alopesia

Kupoteza nywele kichwani tatizo linalojulikana kama alopesia limetokana na neno la Kilatini “alopex” linalomaanisha mbwamwitu, limetumika kumaanisha tatizo hili kwa sababu ya mbwa hawa kuwa na sehemu zenye upara kwenye miili yao.

Alopesia ni tatizo linalofahamika sana kwa wanaume na huonekana ni tatizo la kawaida. Tafiti za kisayansi zinaonyesha kuwa tatizo hili huambatana na kiwango kikubwa cha homoni ya  testosterone kwenye shina la nywele wakati huo kiwango hiko huwa cha kawaida kwenye damu.

Kuna aina mbili za tatizo la alopesia alopesia inayoathiri kichwa kizima na alopesia inayoathiri eneo dogo la kichwa, aina hizi zinaweza pia huweza kuwapata watoto na wanawake. Alopesia inaweza kuathiri sehemu moja na ndogo ya kichwa au kichwa kizima.

 

Mvurugikko kwenye mzunguko wa ukuaji wa nywele unaosababisha alopesia hutokea huchangiwa na sababu mbalimbali kama mvurugiko wa homoni mwilini, matumizi ya dawa aina Fulani, magonjwa ya Ngozi ya michomo kutokana na kinga za mwili kwenye mashina ya nywele na msongo mwilini kutokana na kuugua au kufanyiwa upasuaji.

 

Visababishi, Vihatarishi, Matibabu na dawa, Pata tiba

Kuendelea kusoma bonyeza kipengele unachotaka kusoma, lakini pia utahitaji kujisajili kwa kutumia barua pepe yako tu. Hakuna malipo kujisajili

Imeboreshwa 20.02.2020

Kupata tiba na dawa Wasiliana nasi ULY CLINIC

 

Rejea

ABCs of dermatology chapisho la 4

Kupoteza nywele kichwani ulycinic
bottom of page