Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Salome A, MD
1 Agosti 2020 16:06:17
Anatomia ya Kinywa
Ni sehemu yenye umbo la mduara ndani ya kichwa, sehemu hii ni muhimu sana katika mwili wa binadamu maana hutumika katika mfumo wa umeng'enyaji wa chakula pamoja na kuongea
Kinywa kimeundwa na sehemu mbalimbali ambazo ni:
Midomo
Hii ni sehemu ya nje ya kinywa inayotumika kufungua na kufunga kinywa, hutumika pia katika utengenezaji wa matamshin na hufahamika kwa jina jingine la lipsi.
Vestibule
Hii ni sehemu yenye tishu laini kati ya midomo na mashavu yenye tezi kwa ajili ya kutoa maji maji kwenye kinywa.
Tundu la mdomo
Sehemu hii imeundwa na meno, Palate laini na ngumu pamoja na ulimi.
Fizi
Sehemu hii imeundwa na tishu ambazo zinashikilia meno
Meno
Meno ya binadamu yapo ya aina mbili ambayo ni meno ya muda mfupi na meno ya muda mrefu ; Meno ya muda mfupi ni meno ambayo huwa unazaliwa nayo na huanza kutoka baada ya miaka 6 hadi 7 na nafasi yake kuchukuliwa na meno ya moja kwa moja
Palate
Sehemu hii imeundwa na palate laini na ngumu ,palate ngumu ni sehemu ya juu ndani ya mdomo na palate laini ni sehemu ambayo ipo karibu na tundu la mdomo na kuelekea kwenye koo.
Ulimi
Ni kiungo ambacho kina misuli bila kuwa na mfupa, kiungo hiki kinatumika kwa ajili ya kuonja ladha,kuongea na kumeza.
Tezi za mate
Hizi ni tezi ambazo zinatumika katika kutoa mate na vimeng'enya ambavyo vinatumika katika kumeng'enya.
Kinywa kimepitiwa na neva kubwa ambayo ni vagus na trigeminal tawi la kati
ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute ushauri kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kaifya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubonyeza 'Pata Tiba' au Mawasilino yetu.
Imeboreshwa,
25 Septemba 2021 10:51:38
Rejea za makala hii,
BetterHealth.Mouth.https://www.betterhealth.vic.gov.au/health/conditionsandtreatments/mouth . Imechukuliwa 1/8/2020
WebMd.Mouth.https://www.webmd.com/oral-health/ss/slideshow-mouth-problems. Imechukuliwa 1/8/2020
Britannica.Mouth.https://www.britannica.com/science/mouth-anatomy . Imechukuliwa 1/8/2020
Cancer. Gov. https://training.seer.cancer.gov/anatomy/digestive/regions/mouth.html. Imechukuliwa 1/8/2020