Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Lugonda M, MD
31 Julai 2020 14:25:46
Anatomia ya Mapafu
Ni ogani muhimu sana katika mfumo wa upumuaji. Mapafu hupatikana ndani ya kifua na katikati hukaliwa na moyo pamoja na mishipa mikubwa ya damu na mirija ya hewa.
Idadi ya mapafu
Mwili wa binadamu una mapafu mawili ambayo ni pafu la kulia na kushoto
Sifa za mapafu
Pafu la kulia ni zito na kubwa kuliko la kushoto na pafu la kushoto ni dogo kutokana na moyo kukalia katika sehemu ya chini ya pafu hili
Mapafu yamezungukwa na ukuta unauoitwa pleural ambao una sehemu kuu mbili visceral na Parietal
Ukuta wa Visceral pleural ni hufunika mapafu
Ukuta wa Parietal Pleural hufunika kuta za ndani ya kifua na ukuta wa dayaframu. Mwonekano wake hufanana na rangi ilivyopakwa kwenye ukuta ndani ndani ya nyumba
Ukuta wa Parietal Pleural imegawanyika katika sehemu kuu nne;
Ukuta wa Coastal pleural
Sehemu hii imezunguka ukuta wa ndani ya kifua sehemu zenye mbavu
Ukuta wa Mediastinal pleural
Huzunguka maeneo ya nje ya ogani zili katikati ya mapafu
Ukuta wa Diaphragmatic pleural
Sehemu hii huzunguka ukuta dayaframu upande wa ndani ya kifua
Ukuta wa Cervical pleural
Ukuta huu imepanuka kuelekea sehemu ya juu ya kifua kwenye mzizi wa shingo
Kila pafu limegawanyika katika vipande vyenye uwezo wa kufanya kazi ya upumuaji wa kujitegemea vinavyoitwa lobes, pafu la kulia lina lobe 3 na pafu la kushoto lina lobe 2
Mirija ya hewa ya mapafu
Mapafu hupokea hewa kutoka nje inayopita katika mdomo au pua kisha kuingia kwenye mrija mkubwa unaoitwa trakea, mrija huu hufanya matawi mawili yanayoitwa Bronkasi, tawi la kushoto na kulia ambayo huingia katika pafu la kulia na pafu la kushoto. Bronkas pia hugawanyika katika matawi kutegemea idadi ya lobe katika mapafu, upande wa kushoto bronchus hugawanyika na kutengeneza bronchiole mbili na upande wa kushoto hutengeneza bronkioli tatu. Bronkioli hugusana moja kwa moja na vifuko vya mapafu vinavyoitwa alviolus ambavyo huwa na kazi kubwa ya kufanya ubadilishanaji wa hewa safi na hewa chafu.
Mishipa inayolisha mapafu
Mapafu yanapata damu kutoka kwenye ateri ya bronkio inayoanzia kwenye aota . Damu hiyo hupeleka damu kwenda kwenye pleura
Arteri pulmonari pia hupeleka damu yenye uchafu kwenye mapafu na ili kuifanya iondolewe uchaafu huo na kupokea hewa safi ya oksijeni
Damu safi yenye oksijeni hutolewa kwenye mapafu kwa kupitia vein za pulmonary kisha kupokelewa na vein bronkio
Mishipa ya fahamu ya mapafu
Mapafu yamepitiwa na neva ya vagus na mfumo wa fahamu wa sympathetiki ambayo husaidia katika upumuaji
ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute ushauri kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kaifya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubonyeza 'Pata Tiba' au Mawasilino yetu.
Imeboreshwa,
25 Septemba 2021 10:50:45
Rejea za makala hii,
Opentext.LungsAnatomy.https://opentextbc.ca/anatomyandphysiology/chapter/22-2-the-lungs/. Imechukuliwa 31/7/2020
WebMd.LungsAnatomy.https://www.webmd.com/lung/picture-of-the-lungs. Imechukuliwa 31/7/2020
TeachMeToday.LungsAnatomy.https://teachmeanatomy.info/thorax/organs/lungs/. Imechukuliwa 31/7/2020
HealthLine.Lungs.https://www.healthline.com/human-body-maps/lung. Imechukuliwa 31/7/2020