Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Benjamin L, MD
27 Oktoba 2020 09:40:14
Mifupa ya mguu
Mguu umegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni :
Paja:
Hii ni sehemu ya juu ya mguu ambayo ipo kati ya jointi ya hips na goti.
Mguu:
Hii ni sehemu ya mguu ambayo ipo kati ya jointi ya goti na jointi ya ankle ambayo ipo karibu na kifundo cha mguu
Kanyagio:
Hii ni sehemu ya chini kabisa ya mguu ambayo ipo chini ya jointi ya ankle ambayo ipo karibu na kifundo cha mguu
Mguu kwa ujumla una mifupa 30 ambayo imegawanyika katika femur, Patella, tibia, fibula, taso, metataso na mifupa ya falanjez
Fima:
Ni mfupa mrefu uliopo kwenye paja ambao ni imara kuliko mifupa yote. Sehemu ya juu ya mfupa huu ambayo ni ya mduara ni kichwa cha femur ambacho huungana na acetabulum ya kwenye nyonga, kutengeneza hips jointi
Sehemu ya chini ya mfupa huu inayo sehemu ambazo ni condyle ya pembeni ya femur na condlyle ya kati ya femur. Hizi zote huungana na tibia kutengeneza jointi ya magotini .Hizi condlyle husaidia katika misuli kujishikiza
Patela:
Ni mfupa ambao umejishikiza kwenye tendon na misuli na kutengeneza jointi. Mfupa huu hupatikana katika tendon za misuli ya quadriceps femoris ambao ni msuli mkubwa katika paja sehemu ya mbele
Tibia:
Ni mfupa wa kati kwenye mguu, mfupa huu ni mkubwa zaidi ya fibula. Mfupa huu husaidia katika kubeba uzito wa mwili , ni mfupa wa pili katika urefu baada ya fima. Sehemu ya juu ya tibia imeundwa na kondaili ya kati na sehemu ya pembeni ya tibia imeundwa na kondaili ya pembeni
Sehemu ya chini ya tibia imeundwa na vifundo vya miguu ambapo kuna kifundo cha mguu cha kati na sehemu ya pembeni kuna nochi ya fibula ambayo huungana na tibia kutengeneza jointi ya tibiofibula
Fibula:
Ni mfupa wa mguu ambao upo pembeni ukilinganisha na radius. Mfupa huu hauhusiki na ubebaji wa uzito bali hutumika kama kishikizo cha misuli. Kichwa cha fibula huungana na tibia kutengeneza jointi ya tibiofibula sehemu ya chini na pembeni ya fibula hutengeneza kifundo cha mguu
Mifupa taso
Mifupa taso ipo mitano ambayo ni talus, calcaneus, cuboid, navicular na cuneiform. Mifupa hii ni sehemu ya mifupa ya kanyagio
Mifupa metataso;
Kanyagio la mguu limeundwa na mifupa ya metataso ambayo ipo kati ya mifupa ya taso na falanjez
Kila mfupa wa metataso kwa mbele zaidi unaungana na falenjiz na kuunda jointi ya Metatasofalinjo
Falanjez:
Hii ni mifupa uliopo kwenye vidole ambapo ipo jumla ya mifupa 14. Kidole gumba kina mifupa miwili ambayo ni mfupa wa juu na wa chini. Vidole vinavyofutia huwa na mifupa mitatu ambayo ni mifupa ya juu,kati na chini
ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute ushauri kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kaifya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kubonyeza 'Pata Tiba' au Mawasilino yetu.
Imeboreshwa,
25 Septemba 2021 10:49:57
Rejea za makala hii,
LowerLimbBone.LumenLearning.https://courses.lumenlearning.com/nemcc-ap/chapter/bones-of-the-lower-limb/. Imechukuliwa 1/10/2020
LowerLimbBone.Opentextbc.https://opentextbc.ca/anatomyandphysiology/chapter/8-4-bones-of-the-lower-limb/. Imechukuliwa 1/10/2020
LowerLimbBone.TeachMeAnatomy.https://teachmeanatomy.info/lower-limb/bones/. Imechukuliwa 1/10/2020
LowerLimbbone.KenHub.https://www.kenhub.com/en/library/anatomy/lower-extremity-anatomy. Imechukuliwa 1/10/2020