top of page

Imeandikwa na daktari wa ulyclinic

 

Ang’zayati

Ang’zayat ni neno la Kiswahili lililotokanana neno la kizungu “anxiety” lililotokana na neno la kiratini anxus likiwa linamaanisha shauku kuu, hofu kuu ya nini kitakachotokea.

Ang’zayati inaweza kuwa ni hali ya kawaida kwa binadamu, na wakati mwingine inaweza ikawa ni ugonjwa wa akili, huweza kusababishwa na msongo wa mawazo, madawa ya kuchangamsha mwili kama amphetamine, kahawa, kokaine, bangi na mengine mengi na madhara ya kuacha dawa hizo, madhaifu ya mfumo wa fahamu, (kama yanayotokana na majeraha ya ubongo, maambukizi, madhaifu ya mfumo wa ndani wa sikio), madhaifu kwenye mfumo wa kadiovasikula(kufeli kwa moyo, arizimiazi) madhaifu ya mfumo wa endokrein(kuzalishwa kwa wingi homoni za thairoidi, adreno, upungufu wa sukari kwenye damu, feokromosaitoma) au kugazilika kwa mfumo wa upumuaji  kutokana na pumu, ugonjwa wa mapafu wa COPD

 

Siku zote muulize daktari wako endapo una dalili hii kwa ushauri, uchunguzi na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri vipimo na tiba bonyeza hapa au piga namba za simu chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa 10.03.2020

 

Rejea

  • Ulyclinic

bottom of page