top of page

Maana

​

Dalili

​

Visababishi

​

Madhara

​

Matibabu

​

Upasuaji

​

Matibabu ya nyumbani

​

Kinga

Imeandaliwa na madaktari wa ULY-Clinic

 

 

 

 

Maana ya Bawasili

​

Bawasiri kwa jina jingine hufahamika kam pile ni vimbe  kwenye mishipa ya damu ya vena iliyopo ndani ya tundu la haja kubwa au chini ya ngozi inayotengeneza mlango wa kutolea kinyesi. Vimbe za mishipa hii inaweza kutokana na;

​

  • Kukenya(kutumia nguvu nyingi/kubwa kusukuma kinyesi) wakati wa kujisaidia haja kubwa au

  • Ongezeko la shinikizo la ndani ya mishipa hii wakati wa ujauzito kama mojawapo ya kisababishi.

 

Bawasiri huweza tokea sehemu ya ndani  ya njia ya haja kubwa ambapo huitwa bawasiri la ndani au nje ya njia ya haja kubwa  na huitwa bawasili la nje

 

Bawasili hutokea sana kwenye umri wa miaka 50, nusu ya watu hawa huwa wanavimba au kuwa na michomo katika mishipa hii ndani au nnje ya puru na huambatana na dalili za kuwashwa, hali isiyo ya kawaida maeneo hayo na kutokwa damu

​

Kwa bahati nzuri kuna matibabu ya aina mbalimbali yanayopatikana kwa ajili ya tatizo hili, wakati mwingine mtu anaweza kupata matibabu ya nyumbani yakiendana na mabadiliko ya mfumo wa maisha.

bottom of page