top of page

Maana

​

Dalili

​

Visababishi

​

Madhara

​

Matibabu

​

Upasuaji

​

Matibabu ya nyumbani

​

Kinga

Matibabu ya Bawasiri mtu anaweza kufanya Nyumbani 

 

Imeandikwa na daktari wa ulyclinic

​

Siku zote unaweza kupuguza maumivu yasiyo makali sana kuvimba na michomo ya bawasili kwa matibabu ya nyumbani. Haya hapa chini ndio matibabu yanayotakiwa;

​

  • Tumia dawa za kupaka-Tumia dawa za kupaka unazonunua dukani zenye kemikali ya hydrocortisoni lakini usitumie kwa muda unaozidi wiki mbili kama maumivu anazidi onana na dakitari. Unaweza kutumia pad zenye kemikali za kuleta ganzi pia ilikupambana na maumivu kiasi 

  • Kalia maji ya vuguvugu kwa ratiba maalumu kwa dakika 10 hadi 15 mara mbili hadi tatu kwa siku

  • Yatunze maeneo ya njia ya haja kubwa na yawe masafi wakati wote tumia vitambaa kukausha majimaji au ukiwa unaoga kila siku safisha maeneo hayo. Sabuni sio lazima kwa sababu huweza kuamsha maumivu. Usiweke kemikali kama spiriti na vitambaa vyenye perfume maana utapata maumivu makali na pia kumbuka kukausha maeneo hayo pindi unapomaliza kuoga

  • Usitumie karatasi za kutawazia zilizo kavu kujitawaza unapotoka chooni. Tumia karatasi ya kutawazia yenye majimaji na isiwe na kemikali zenye marashi au spirit

  • Weka ubaridi kama barafu kwenye njia ya haja kubwa kupooza maumivu

  • Tumia dawa za kutuliza maumivu kama paracetamo , aspirini, ibuprofen

​

Kwa matibabu hayo maumivu ya bawasili maranyingi hupotea ndani ya muda wa wiki moja tu. kumbuka kumwona dakitari kama maumivu yanaendelea, kuwa makali au unatokwa na damu

​

Imeboreshwa 5/01/2022

bottom of page