top of page

Nini husabisha Bawasiri

 

Imeandkwa na daktari wa ulyclinic

 

Mishipa inayozunguka mlango wa kutolea haja kubwa hutanuka kukiwa na shinikizo kubwa/ mgandamizo na hivo huweza kujaa au kuvimba kutokana na kuwepo kwa damu ndani yake. Mishipa iliyovimba maeneo haya huitwa bawasiri.

 

Vitu vifuatavyo vinaweza kuongeza shinikizo maeneo hayo kisha kusababisha mishipa hii kuvimba;

  • Kukenya wakati wa kujisaidia (kutumia nguvu nyingi wakati wa kutoa haja kubwa 

  • Kukaa muda mrefu chooni unapokuwa unajisaidia 

  • Kuhara kwa muda mrefu au choo kigumu

  • Uzito mkubwa kupita kiasi

  • Ujauzito

  • Kuingiliwa kinyume na maumbile

  • Kutokula chakula chenye nyuzilishe za kutosha

Bawasili hutokea sana kwa watu wazima au wanaapokuwa wazee maana kuta zinazozuia mishipa hii huvutika na kutanuka jinsi mtu anavyokuwa mzee

Imeboreshwa 05/01/2022

bottom of page