top of page

Unawez akuzuia bawasiri?

 

Imeandikwa na daktari wa ulyclinic

Njia nzuri ya kuzuia au kujikinga na bawasili ni kufanya choo chako au kinyesi chako kuwa laini, kwamba kitapita kirahisi ukiwa unatoa haja kubwa. Kujikinga au kuzuia dalili za bawasili unaweza kufanya yafuatayo;

  • Kula chakula chenye nyuzinyuzi kwa wingi. Kula matunda mengi, mboga za majani na vyakula visivyokobolewa. Kwa kufanya hivo unaongeza uzito wa kinyesi na kufanya kiwe rahisi kupita na kuzuia kukenya-straining wakati wa kujisaidia haja kubwa ambako kunakuweka hatarini kupata bawasili au kusumbuliwa na bawasili hata kama umeshapata. Ongeza mboga za majani kwa kiwango kidogo kidogo ili uepukane na kupata gesi tumboni.

  • Kunywa maji ya kutosha, glasi 6 hadi 8 za maji kila siku au vinywaji vingine isipokuwa pombe ili kufanya choo/kinyesi kiwe laini.

  • Pata kiwango cha nyuzilishe kama dawa. Watu wengi hawapati kiwango cha nyuzinyuzi kwenye chakula, kinachohitajika hasa maeneo ya mjini na nchi zilizoendelea kutokana na gharama. Mwanamke anatakiwa kupata gramu 25 na mwanaume gramu 38 za nyuzinyuzi kila siku katika chakula wanachokula.

  • Tafiti zinaonyesha kwamba nyuzilishe zinazopatikana kama dawa zinazouzwa kwenye maduka ya dawa husaidia kupunguza dalili za ugonjwa wa bawasili.Lakini inashauliwa kama inawezekana kupata nyuzinyuzi hizi kutoka kwenye matunda na mbopgamboga za majani kwani huwa hazina madhara. 

Kama unatumia nyuzilishe hizi za kununua basi kumbuka kunywa maji mengi (glasi 6 hadi 8) au vinywaji vingine kila siku, vinginevyo nyuzinyuzi hizi zinaweza kusababisha choo kigumu au kusababisha tatizo la choo kigumu kuwa kubwa zaidi

  • Usikenye-usitumie nguvu nyingi wakati wa kujisaidia haja kubwa. Kukenya na kubana pumzi unapokuwa unatoa kinyesi mkunduni huongeza shinikizo kwenye mishipa iliyo mkunduni na hivo mtu anaweza kupata bawasili. 

  • Nenda chooni mara unapopata hisia ya kwenda haja kubwa. Kama ukijizuia kwenda chooni unapopata hisia, kinyesi huwa kigumu na Hupita kwa shida baadae

  • Fanya mazoezi. fanya mazoezi kuzuia choo kigumu na kupunguza shinikizo ndani ya mishipa ya mkunduni. mazoezi yanaweza kusababisha upungue uzito kupita kiasi unaoongeza kupata bawasili.

  • Usikae sana kwa muda mrefu. Kukalia matako kwa muda mrefu hasa chooni  kunaongeza shinikizo kwenye mishipa iliyopo mkunduni

Reje za mada hii

  1. Davis BR, et al. The American Society of Colon and Rectal Surgeons clinical practice guidelines for the management of hemorrhoids. Diseases of the Colon and Rectum. 2018;61:284.

  2. Definition & facts of hemorrhoids. National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases. https://www.niddk.nih.gov/health-information/digestive-diseases/hemorrhoids/symptoms-causes. Imechukuliwa 02.91.2022

  3. What are hemorrhoids? The American Society of Colon and Rectal Surgeons. https://www.fascrs.org/patients/disease-condition/hemorrhoids-expanded-version. Imechukuliwa 02.91.2022

  4. Kellerman RD, et al. Hemorrhoids, anal fissure, and anorectal abscess and fistula. In: Conn's Current Therapy 2019. Philadelphia, Pa.: Elsevier; 2019. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 02.91.2022

  5. Bleday R, et al. Home and office treatment of symptomatic hemorrhoids. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 02.91.2022

  6. Brown AY. AllScripts EPSi. Rochester, Minn. Imechukuliwa 02.91.2022

bottom of page