
Bei ya Bisoprolol
Bisoprolol ni dawa ya kundi la vizuia beta chaguzi(β1-selective) inayotumika kudhibiti shinikizo la damu (presha), magonjwa ya moyo, mapigo ya moyo kwenda kasi (tachycardia), na moyo kushindwa kufanya kazi (kuferi kwa moyo) kwa baadhi ya wagonjwa. Hufanya kazi kwa kupunguza kasi na nguvu ya mapigo ya moyo.
Fomu za kawaida za Bisoprolol
Bisoprolol kidonge cha 2.5 mg
Hutumika sana kuanza matibabu au kwa wagonjwa wa moyo kushindwa kufanya kazi.
Bisoprolol kidonge cha 5 mg / 10 mg
Hutumika kudhibiti presha na matatizo mengine ya moyo.Dozi ya kawaida: mara 1 kwa siku.
Bei
MSD / Bohari ya dawa: TZS 500–1,200 kwa pakiti ya vidonge
Famasi binafsi: TZS 1,500–3,500 kwa pakiti ya vidonge (kulingana na dozi na chapa)
Kumbuka muhimu
Usisimamishe dawa ghafla; inaweza kusababisha mapigo ya moyo kwenda kasi au presha kupanda
Inaweza kusababisha kizunguzungu, uchovu, mapigo ya moyo kuwa polepole
Tumia kwa tahadhari kwa wagonjwa wenye pumu au matatizo ya mapafu
Inashauriwa kupima presha na mapigo ya moyo mara kwa mara
Tumia chini ya ushauri wa mtaalamu wa afya
Imeboreshwa:
20 Januari 2026, 14:12:15
