top of page
Bei ya Cetirizine

Bei ya Cetirizine

Cetirizine ni dawa ya kundi la antihistamines (kizuia H1 ) inayotumika kupunguza dalili za mzio kama vile kukohoa kwa mzio, mafua ya mara kwa mara (allergic rhinitis), kuwashwa ngozi, kuvimba ngozi(yutikaria), macho kuwasha na kupiga chafya. Ni dawa ya kizazi cha pili, hivyo husababisha usingizi kidogo ukilinganisha na antihistamine za zamani.


Fomu za kawaida za Cetirizine


Cetirizine kidonge cha 10 mg

Hutumika kwa watu wazima na watoto wakubwa. Dozi ya kawaida: kidonge 1 mara 1 kwa siku (hasa jioni).


Cetirizine syrup (5 mg/5 ml)

Hutumika kwa watoto. Dozi hutegemea umri na uzito wa mtoto.


Bei

MSD / Bohari ya dawa: TZS 300–700 kwa pakiti ya vidonge

Famasi binafsi: TZS 800–2,000 kwa pakiti ya vidonge

Cetirizine ya maji: TZS 3,000–6,000 kwa chupa (kutegemea ujazo na chapa)


Kumbuka Muhimu

  • Inaweza kusababisha usingizi mdogo, kinywa kukauka au kizunguzungu kwa baadhi ya watu

  • Epuka kuendesha gari au mashine nzito endapo itakusinzisha

  • Inaweza kutumiwa kwa watoto lakini kwa dozi sahihi kulingana na umri

  • Ni salama kwa matumizi ya muda mfupi na mrefu chini ya ushauri wa mtaalamu

  • Si dawa ya kutibu chanzo cha mzio, bali hupunguza dalili

Imeboreshwa:

15 Januari 2026, 08:53:37

bottom of page