
Bei ya Diclofenac
Diclofenac ni dawa ya kundi la dawa za kutuliza maumivu jamii ya NSAID inayotumika kupunguza maumivu makali, uvimbe na uchochezi. Hutumika sana kwa maumivu ya viungo (Athraitis), mgongo, misuli, maumivu baada ya upasuaji, maumivu ya hedhi, pamoja na majeraha ya mifupa na viungo.
Fomu za kawaida za Diclofenac
Diclofenac vidonge (Tablets) 50 mg
Hutumika kwa watu wazima.Dozi ya kawaida: 50 mg mara 2–3 kwa siku (usizidi 150 mg kwa siku).
Bei:
MSD / Bohari ya Dawa: TZS 300–700 kwa pakiti
Famasi binafsi: TZS 500–2,000 kwa pakiti (kulingana na chapa)
Diclofenac ya sindano (Injection 75 mg/3 ml)
Hutumika hospitalini au vituo vya afya kwa maumivu makali ya ghafla.
Bei:
MSD / Bohari ya Dawa: TZS 800–1,500 kwa dozi
Hospitali / Famasi binafsi: TZS 1,500–3,500 kwa dozi (bila gharama ya huduma)
Diclofenac ya krimu au jeli (Topical 1%–2%)
Hupakwa juu ya ngozi kwa maumivu ya misuli na viungo.
Bei:
Famasi binafsi: TZS 3,000–8,000 kwa tube
Diclofenac ya tembe za kuweka njia ya haja kubwa (50 mg / 100 mg)
Hutumika kwa wagonjwa wasioweza kumeza dawa au kwa maumivu ya usiku.
Bei:
Famasi binafsi: TZS 2,000–5,000 kwa pakiti
Kumbuka Muhimu
Diclofenac itumike baada ya chakula ili kulinda tumbo
Inaweza kusababisha vidonda au kuvuja damu tumboni
Epuka matumizi ya muda mrefu bila uangalizi wa daktari
Haipendekezwi kwa wagonjwa wa vidonda vya tumbo, figo au moyo
Haifai kwa wajawazito hasa kipindi cha mwisho cha ujauzito
Imeboreshwa:
14 Januari 2026, 11:33:11
