top of page

Bei ya Fosfomycin
Fosfomycin ni antibiotiki inayotumika hasa kutibu maambukizi ya njia ya mkojo (UTI) yasiyo makali, hususan homa ya kibofu cha mkojo(sistaitis), kwa wanawake na wanaume. Ina faida ya kutumika kwa dozi moja na hufanya kazi dhidi ya bakteria wengi sugu.
Fomu za kawaida za Fosfomycin
Fosfomycin sachet 3g (poda ya kunywa)
Hutumika kwa watu wazima. Dozi ya kawaida: dozi moja tu (3g), huchanganywa na maji na kunywa mara moja
Bei:
Famasi binafsi: TZS 8,000–15,000 kwa sachet moja (kulingana na chapa na eneo)
Kumbuka Muhimu
Fosfomycin si dawa ya fangasi, ni ya bakteria pekee
Hutumika kwa UTI rahisi tu, si kwa maambukizi ya figo au damu
Inashauriwa kunywa usiku kabla ya kulala baada ya kukojoa
Haitakiwi kutumiwa bila ushauri wa mtaalamu wa afya
Matumizi mabaya ya antibiotiki huchangia usugu wa dawa
Imehuishwa:
11 Januari 2026, 06:45:57
bottom of page
