
Bei ya Hydrochlorothiazide
Hydrochlorothiazide (HCTZ) ni dawa ya kundi la thiazide dyuuretiki inayotumika kupunguza shinikizo la damu kwa kusaidia figo kutoa chumvi na maji mengi mwilini kupitia mkojo. Pia hutumika kutibu uvimbe (edema) unaosababishwa na magonjwa ya moyo, figo, au ini, na mara nyingi huunganishwa na dawa nyingine za presha.
Fomu za kawaida za Hydrochlorothiazide
Hydrochlorothiazide vidonge (12.5 mg / 25 mg / 50 mg)
Hutumika kwa wagonjwa wa nje.Dozi ya kawaida: 12.5–25 mg mara 1 kwa siku (asubuhi).
Bei:
MSD / Bohari ya dawa: takriban TZS 100–250 kwa kidonge
Famasi binafsi: takriban TZS 300–700 kwa kidonge
Kumbuka muhimu
HCTZ husababisha kukojoa zaidi, hasa mwanzoni mwa matibabu
Inaweza kupunguza kiwango cha potassium (potasium) mwilini
Wagonjwa wa kisukari huweza kuona ongezeko la sukari kwenye damu
Inashauriwa kunywa asubuhi ili kuepuka kukojoa sana usiku
Haitakiwi kutumiwa bila ushauri wa mtaalamu wa afya
Imeboreshwa:
15 Januari 2026, 08:34:17
