
Bei ya Levonorgestrel (P2)
Levonorgestrel (P2) ni dawa ya homoni inayotumika kama dawa ya dharura ya kuzuia mimba (vidonge vya dharura vya uzazi wa mpango). Hutumiwa ndani ya masaa 72 baada ya tendo la ngono bila kinga ili kuzuia mimba kutokea. Inajulikana sana kwa jina la biashara P2 au Postinor-2.
Fomu za kawaida za Levonorgestrel (P2)
Levonorgestrel tembe (0.75 mg × 2)
Hii ndiyo fomu ya kawaida zaidi. Hutolewa kama vidonge viwili vya 0.75 mg (jumla 1.5 mg), vinavyoweza:
kumezwa kwa pamoja mara moja, au
kimoja kimoja kwa tofauti ya masaa 12 (kulingana na mwongozo wa kitabibu).
Bei ya Levonorgestrel (P2)
MSD / Bohari ya dawa (Serikali)
Levonorgestrel (P2) haipatikani kama dawa ya kawaida ya MSD kwa matumizi ya mtu mmoja mmoja.
Mara nyingi hupatikana kupitia programu za uzazi wa mpango kwenye vituo vya serikali kama huduma ya uzazi wa mpango.
Famasi binafsi / soko la wazi
P2 / Postinor-2 (vidonge 2 vya 0.75 mg): takriban TZS 5,000 kwa pakiti 1 (bei ya famasi binafsi na wauzaji wa dawa mtandaoni Tanzania)
Bei hutegemea:
Chapa ya dawa (mf. Postinor-2, Emerginor, n.k.)
Famasi / mtoa huduma
Mkoa ulipo
Upatikanaji wa dawa
Mambo muhimu kufahamu kuhusu Levonorgestrel (P2)
P2 ni dawa ya dharura, si dawa ya kawaida ya uzazi wa mpango
Hatoi mimba iliyokwisha tungwa
Hufanya kazi kwa:
kuchelewesha uovuleshaji
kuzuia mbegu kurutubisha yai
Haipaswi kutumika mara kwa mara kama njia ya kawaida ya uzazi wa mpango
Inaweza kusababisha:
kichefuchefu
mabadiliko ya hedhi
maumivu ya kichwa
kizunguzungu
Imeboreshwa:
25 Januari 2026, 09:13:30
