top of page
Bei ya Magnesium trisilicate

Bei ya Magnesium trisilicate

Magnesium trisilicate ni dawa ya kupunguza asidi tumboni inayotumika kutibu:

  • Kiungulia

  • Asidi nyingi tumboni

  • Vidonda vya tumbo kama tiba saidizi

  • Maumivu ya tumbo yanayosababishwa na asidi

Ni dawa inayotumika sana katika huduma za msingi za afya.


Fomu za kawaida za Magnesium Trisilicate


1. Magnesium trisilicate tembe (kidonge cha kutafuna)

Hutumika zaidi kwa watu wazima.Tembe hutafunwa kabla ya kumezwa.


Bei za Magnesium Trisilicate kwa mujibu wa MSD


Magnesium Trisilicate Tembe – MSD

Kifungashio (MSD)

Bei ya MSD

Bei kwa tembe 1 (makadirio)

Pakiti ya tembe 100

TZS 3,000 – 5,000

~TZS 30 – 50

Hizi ndizo bei rasmi za Bohari ya dawa (MSD) zinazotumika kwenye hospitali na vituo vya afya vya serikali.

Bei za Magnesium Trisilicate kwenye Maduka ya dawa binafsi (Makadirio ya soko)

Fomu

Bei ya Kawaida

Magnesium trisilicate (tembe 1)

TZS 300 – 800

Pakiti ndogo (tembe 10)

TZS 3,000 – 7,000

Bei hutofautiana kulingana na chapa ya dawa, eneo la famasi na upatikanaji wa dawa kutoka MSD.

Fomu nyingine zinazopatikana


2. Magnesium trisilicate suspension (maji)

Hutumika zaidi kwa wagonjwa wasioweza kutafuna tembe au wenye maumivu makali ya tumbo.

Kifungashio

Bei ya MSD (wastani)

Bei ya Famasi Binafsi

Chupa (200–300 ml)

TZS 2,000 – 4,000

TZS 4,000 – 8,000


Muhimu kuhusu Bei na matumizi ya Magnesium Trisilicate

  • Magnesium trisilicate ni dawa ya kupunguza asidi, si antibiotiki

  • Tumia kwa muda mfupi kulingana na maelekezo

  • Tenganisha muda wa kunywa na dawa nyingine (angalau saa 2)

  • Bei ya MSD ni nafuu zaidi na ndiyo rejea ya gharama halisi

Imeboreshwa:

16 Januari 2026, 09:40:13

bottom of page