
Bei ya Prednisolone
Prednisolone ni dawa ya kundi la corticosteroids inayotumika kupunguza uvimbe kinga (inflamesheni), mzio (aleji), na kukandamiza mwitikio wa kinga ya mwili. Hutumika kwenye magonjwa mengi kama pumu kali, magonjwa ya ngozi, magonjwa ya macho, maungio kama magoti (arthraitis), magonjwa ya utumbo (kama kolaitis ya vidonda), na baadhi ya magonjwa ya damu na kinga.
Fomu za kawaida za Prednisolone
Prednisolone kidonge cha 5 mg / 10 mg / 20 mg
Hutumika kwa watu wazima na watoto (kwa dozi maalum). Dozi hutegemea ugonjwa inaweza kuwa ya muda mfupi au mrefu kulingana na maelekezo ya daktari.
Prednisolone syrup (maji) – kwa watoto
Hutumika kwa watoto au wagonjwa wasioweza kumeza vidonge.
Bei
MSD / Bohari ya dawa: TZS 200–600 kwa pakiti ya vidonge (hutegemea dozi na idadi)
Famasi binafsi: TZS 500–1,500 kwa pakiti ya vidonge
Prednisolone ya maji: TZS 3,000–7,000 kwa chupa, kulingana na ujazo na chapa
Kumbuka muhimu
Prednisolone isitumike bila ushauri wa daktari, hasa kwa matumizi ya muda mrefu
Usisimamishe dawa ghafla kama umetumia kwa muda mrefu; hupunguzwa taratibu (kupunguza dozi bila kuachishwa ghafla)
Inaweza kusababisha madhara kama:
Kuongezeka uzito
Kupanda sukari ya damu
Kupanda presha
Vidonda vya tumbo
Kinga kushuka
Tumia kwa tahadhari kwa wagonjwa wa kisukari, presha, vidonda vya tumbo, na maambukizi
Imeboreshwa:
15 Januari 2026, 08:48:04
