top of page
Bei ya Vancomycin

Bei ya Vancomycin

Vancomycin ni antibiotiki ya kundi la glycopeptides yenye nguvu kubwa inayotumika kutibu maambukizi makali ya bakteria sugu, hasa MRSA, Enterococcus, na maambukizi makali ya damu (kusambaa kwa sumu ya bakteria kweye damu au sepsis), homa ya uti wa mgongo (meninjaitis), mapafu na mifupa. Hutumika zaidi hospitalini chini ya uangalizi wa karibu.


Fomu za kawaida za Vancomycin


Vancomycin ya sindano (Injection 500mg / 1g)

Hutumika kwa watu wazima na watoto

Dozi ya kawaida: mara 1–2 kwa siku (hutegemea uzito na kazi ya figo)


Bei:

  • MSD / Bohari ya Dawa: TZS 15,000–30,000 kwa dozi

  • Hospitali / famasi binafsi: TZS 30,000–70,000 kwa dozi (bila gharama ya huduma)


Vancomycin ya kunywa (Oral capsule/solution)

Hutumika maalum kwa maambukizi ya utumbo (C. difficile colitis)


Bei:

  • Famasi binafsi: TZS 40,000–80,000 (kutegemea fomu na dozi)


Kumbuka Muhimu

  • Vancomycin si dawa ya fangasi, ni ya bakteria pekee

  • Hutumika kwa maambukizi makali na sugu pekee, si chaguo la kwanza

  • Inahitaji ufuatiliaji wa karibu wa figo na kiwango cha dawa (drug levels)

  • Inaweza kusababisha Red Man Syndrome endapo itachomwa haraka

  • Haitakiwi kutumiwa bila ushauri na uangalizi wa mtaalamu bingwa

  • Matumizi mabaya ya antibiotiki huchangia usugu wa dawa

Imehuishwa:

11 Januari 2026, 06:50:16

bottom of page