top of page

Imeandikwa na madaktari wa ULY-Clinic

 

Midomo ya bluu kwa mtoto- kisababishi

 

Rangi ya bluu kwenye midomo ya mtoto huweza kumaanisha kuna shida katika mfumo wa hewa au mfumo wa moyo na mishipa ya damu, hapa tutaangalia vitu vinavyoweza kusababisha rangi ya bluu kewnye macho, ulimi na midomo kwa mtoto mdogo au kichanga.

 

Visababishi vya rangi ya bluu mwili mzima huwa joto la chini sana kwa mtoto, kiwango cha chini sana cha sukari, sumu za bakteria katika damu au mshituko wa damu

 

Sababu za kimfumo wa fahamu- homa ya uti wa mgongo, kusimama kupumia, upumuaji mdogo kutokana na tatizo katika mfumo wa kati wa upumuaji, kuvia kwa damu kwenye vyumba wazi vya ubongo.

Mfumo wa upumuaji- shinikizo la damu la juu katika mfumo wa upumuaji kwa vichanga(PPHN), henia kwenye ukuta wa diaframu, kutofanyika kamili kwa mapafu, hewa kuingia kwenye uwazi wa pleura, kuingia kwa kinyesi cha kwanza kwenye mfumo wa hewa,  kipindi cha mpito cha kupumua kwa haraka haraka kwa mtoto.

Matatizo ya moyo- kufeli kusukuma damu kwa moyo, magonjwa ya kuzaliwa yanaayosababisha rangi ya blue(Tetralogy of fallot, truncus ateriosus, total anomalous pulmonary vein return, tricuspid atresia, transposition of great artery)

Matatizo ya damu- polycythemia, methemoglobinemia

Madawa- madawa ya kupunguza upumuaji kutoka kwa mama kama(magnesium sulphate na madawa aina ya narcotic)

 

 

Matibabu na uchunguzi wasiliana na daktari wako au tutafute katika mawasiliano yetu hapo chini

 

 

 

Imechapishwa 3/3/2016

bottom of page