Imeandikwa na Daktari wa ULY-clinic
Bradikadia
Bradikadia ni neno la Kiswahili lillotoholewana ULY clinic kutoka neno tiba bradycardia ambali pia lilitokana na neno la kigiriki braduskadia. “Bradus” ikiwa inamaana “taratibu” na “kadius” likiwa na maana “moyo” hivyo hutumika katika tiba kumaanisha mapgo ya moyo kwenda taratibu. Mapigo ya moyo kwenda taratibu humaanisha mapigo ya moyo kwenda chini ya mapigo sitini(60) kwa kila dakika moja.
Bradikadia huweza kusababishwa na sababu zinazohusiana na moyo au zisizohusiana na moyo.
Visababishi vinavyohusiana na moyo moja kwa moja ni moyo ni pamoja na;
-
Infaksheni ya mayokadia
-
Iskemia ya mishipa ya moyo
-
Sakoidosis
-
Amailoidosis
-
Hemakromatosis
-
Magonjwa ya kolajeni
-
Majeraha ya upasuaji
-
Endokadaitis
-
Ugonjwa wa Myotonic muscular dystrophy
Magonjwa nje ya moyo ni kama;
-
Sindromu zilizoamshwa na mfumo wa autonomiki kama kutapika, kukohoa, kukojoa, kujisaidia haja kubwa n.k
-
Kuongezeka hisia za sinas ya carotid,
-
Dawa mfano jamii ya beta bloka, kalsimu channel bloka, clonidine, digoxin,antarizimic,
-
Magonjwa ya homoni mfano haipothairoidizimu
-
Hypothemia
-
Magonjwa ya nuroni yanayodhuru mfumo wa autonomiki
-
Kutobalance kwa madini mwilini mfano (haipokalemia, haipakalemia)
Imeboreshwa 11.03.2020
Muulize daktari wako endapo una dalili hii kwa ushauri, uchunguzi na tiba.
Rejea
-
Understanding Neuromuscular Disease Care. IQVIA Institute. Parsippany, NJ. (2018).
-
Magee, A. & Nevin, N. C. The Epidemiology of Myotonic Dystrophy in Northern Ireland. Public Health Genomics (2003). doi:10.1159/000016209
-
Siciliano, G. et al. Epidemiology of myotonic dystrophy in Italy: Re-apprisal after genetic diagnosis. Clin. Genet. (2001). doi:10.1034/j.1399-0004.2001.590508.x
-
Norwood, F. L. M. et al. Prevalence of genetic muscle disease in Northern England: In-depth analysis of a muscle clinic population. Brain (2009). doi:10.1093/brain/awp236