Kupata tiba
Utangulizi
Vihatarishi
Dalili
Vipimo
Matibabu
Homa ya matumbo-Taifodi
Ugonjwa wa taifodi au homa ya matumbo ni ugonjwa unaodhuru viungo mbalimbali mwilini lakini huanza tumboni, ugonjwa huu husababishwa na bakiteria anaeitwa salmonella typhi na wakati mwingine salmonella paratyphi
Vimelea hawa wanapokua kwenye tumbo husafiri kwenye mishipa ya damu na kufika sehemu mbalimbali za mwili kama mifupa, ini bandama, na kisha huzaliana kwa wingi ndani ya chembe hai nyeupe za damu zinazolinda mwili ilizopo kwenye mifupa, Ini, bandama na mitoki. Mara baada ya kuendelea kuzaliana katika chembe hizi zinazolinda mwili, chembe hupasuka na bakteria hutolewa kwa wingi na kuvamia maeneo mengi ya mwili na kusabaisha dalili mbalimbali
Vimelea wa kusababisha taifodi hutunzwa na binadamu pamoja ambapo wakati huu mtu anakuwa hana dalili zozote za maambukizi. Endapo mbebaji atajisaidia na itakotea kinyesi chake kimechanganyika na maji basi hata maji yanayotumika kuandalia chakula au kunywa endapo hayajachemshwa vyema mtu anaeza kupata maambukizi ya vimelea wa taifodi
Ndege pia huwa na vimelea hawa wa taifodi( hasa ndege jamii ya kuku). Mtu anaweza kupata vimelea wa Taifodi endapo atakula mayai mabishi au ambayo hayajachemshwa vema.
Je kuna vihatarishi vya kupata ugonjwa huu?
Vimelea vya ugonjwa huu havina kiumbe kingine kinachoweza kuvisafilisha isipokuwa binadamu
Njia zifuatazo husafilisha kimelea huyu;
-
Kula vyakula na vinywaji vilivyotengenezwa na mtu mwenye taifodi( akiwa haoneshi dalili yoyote au anaonesha dalili) ambaye anasambaza vimelea kupitia kinyesi kama asipozingatia usafi wa kunawa mikono au kwa nadra sana mkojo
-
Kutofanya usafi wa mikono( kuto nawa mikono baada ya kutoka chooni)
-
Kula chakula kilichochanganyika na kinyesi kutokana na mifumo mibaya ya maji taka( maji taka kuelekezwa kwenye maji safi wanayotumia binadamu, kujisaidia kwenye vyanzo vya maji) au magamba ya samaki
-
Kula mayai ya ndege(kuku) ambayo hajayaiva vema au nyama isiyoiva vema
-
Kula chakula au kuandaliwa chakula na mtu ambaye anatunza kuku na kuku hao wameathirika na taifodi
Vimelea hawa wa taifodi huweza kuishi hadi kwenye tindikali iliyopo tumboni kwa kuvumilia kidogo na wengine hufa, lakini dawa za kuzuia uzalishaji tindikali tumboni (ant acid) huweza kuongeza kuishi kwa vimelea na kusambaa. Watoto wengi walio shuleni na watoto wadogo wapo hatarini kupata ugonjwa huu na dalili zao huwa hazifanani sana na ugonjwa huu. Wanaweza kupata homa kiasi au kifafa na wakati mwingine hawana dalili zozote mpaka vipimo vifanyike
Zipi ni dalili za ugonjwa wa taifodi?
Dalili za taifodi inayosababishwa na S.typhi na s.paratyphi hazitofautiani sana, hutokea siku 7-14 baada ya kuambukizwa na huwa kama ifuatavyo
-
Homa inayoongezeka siku nzima na kupungua asubuhi inayofuata
-
Baada ya wiki moja ya ugonjwa huu mabadiliko ya tumboni yanatokea kama
-
Maumivu sehemu zote za tumbo na maumivu tumbo likiguswa
-
Maumivu ya kuchoma sehemu ya kulia ya juu ya kitovu
-
Choo kigumu au kukosa choo kabisa wakati wote wa ugonjwa
-
-
Mgonjwa ndipo anaweza kupata kikohozi kikavu, maumivu kiasi mbele ya kichwa ugonjwa wa kupungua fahamu kutokana na kuharibika kwa ubongo(derilium) na kuchoka sana
Baada ya wiki ya kwanza kuisha,
-
joto kupanda na kushuka 39-40 C.
-
Mgojwa anaweza kupata mabaka madogo madogo mwilini na kuisha ndani ya siku 2-5.
Baada ya wiki mbili dalili hizo hapo juu huongezeka maradufu
-
Tumbo huvimba na kuwa kubwa, bandama kuvimba hutokea maranyingi
-
mapigo ya moyo kwenda polepole
Wiki ya tatu mtu anakosa hamu ya kula na mgonjwa anazidi kuwa na hali mbaya zaidi na kupoteza uzito
-
Maambukizi kwenye sehemu nyeupe ya jicho(conjuciva hutokea )
-
pia mgonjwa anaweza kupata shida ya kupumu, kupumua haraka haraka na pia anakuwa na sauti kwenye mapafu endapo atasikilizwa na dakitari, wakati mwingine mgojwa anapata choo chenye rangi ya kijani na njano , kuharisha na kuchanganyikiwa. Wakati mwingine utumbo unaweza kutobolewa na waudu hawa
Ikiwa mtu amepitia kipindi hiki cha wiki nne bila matibabu, homa, tumbo kuvimba na kutojitambua huweza kupotea polepole lakini wakati mwingine mfumo wa fahamu unaweza kuhalibiwa usijirudie hali ya mwanzo
Vipimo gani vinaweza kufanyika kwa mtu akifika hospitali?
Vipimo mbalimbali vinaweza kufanyika kama
-
Kukuza vimelea, huchukuliwa kwenye mifupa na na kuotesha (culture) ambachoo hugundua kimelea huyu kwa asilimia 100. Mkojo na kinyesi maranyingi havitumiki kwa sababu uwezo wa kumtambua kimelea huyu ni mdogo
-
Damu inaweza kutumika kufanya kipimo hiki ka kukuza vimelea hivo
-
Kipimo cha PCR kinachogundua vinasaba vya kimelea husika
Imechapishwa 3/3/2015
Imeboreshwa 12/11/2018