Imeandikwa na ULY CLINIC
20 Septemba 2021, 16:02:05
Prostaitiz sugu

Prostaitiz sugu ni michomo kwenye tezi dume inayotokana na shambulio la kinga kwenye vimelea walio kwenye tezi dume, shambulio hilo hudumu angalau kwa muda wa miezi mitatu na kuendelea.
Prostaitiz sugu licha ya kutoonyesha dalili mara nyingi, huweza kusababisha kutokwa na uchafu mwembamba, kama maziwa na wakati mwingine huwa na weupe wa maji na unaonata.
Uchafu huu huonekana kwenye tundu la uume muda baada ya kuwa na kipindi cha muda mrefu kati ya kenda haja moja ndogo na nyingine kama vile asubuhi.
Dalili
Dalili zinazoweza kuambatana ni
Maumivu butu ndani ya puru na tezi dume
Maumivu wakati wa kutoa shahawa
Kukojoa mara kwa mara
Kushindwa zuia mkojo
Maumivu wakati wa kukojoa
Visababishi
Kuna sababu mbalimbali zimeelezewa kuchangia prostaitiz sugu ambazo ni;
Maambukizi ya kujirudia katika njia ya mkojo haswa yale yanayosababishwa na bakteria kama E. Coli, Enterococci, Pseudomonas, Klebsiella, Proteus, Chlamydia, Ureaplasma, enterobactericeae.
Uchokozi wa kemikali kwenye tezi
Madhaifu kutokana na kukojoa kwa shinikizo kubwa kutokana kuziba kwa njia ya hewa n.k
Kucheuliwa kwa mkojo ndani ya mirija ya tezi dume
Madhaifu ya mfumo wa fahamu na misuli
Magonjwa ya shambulio binafsi la kinga za mwili
Interstitial sistaitiz
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
7 Februari 2022, 19:19:39
Rejea za mada hii
Prostate Cancer Foundation. Prostatitis. https://www.pcf.org/about-prostate-cancer/what-is-prostate-cancer/prostate-gland/prostatitis/. Imechukua 20/09/2021
National Kidney and Urological Diseases Information Clearinghouse. Prostatitis: Inflammation of the prostate. https://www.niddk.nih.gov/health-information/health-topics/urologic-disease/prostate-problems/Pages/facts.aspx/. Imechukua 20/09/2021
JAMES D. HOLT, MD, et al. Common Questions About Chronic Prostatitis. https://www.aafp.org/afp/2016/0215/p290.html. Imechukua 20/09/2021
Vaidyanathan, et al. “Chronic prostatitis: Current concepts.” Indian journal of urology : IJU : journal of the Urological Society of India vol. 24,1 (2008): 22-7. doi:10.4103/0970-1591.38598
Nickel, J Curtis. “Prostatitis.” Canadian Urological Association journal = Journal de l'Association des urologues du Canada vol. 5,5 (2011): 306-15. doi:10.5489/cuaj.11211