top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

6 Mei 2020 10:25:06

Komahedhi
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Komahedhi

Mwanamke mwenye umri kati ya miaka 45 hadi 55 huwa kwenye koma hedhi kama ameacha kuona damu ya mwezi kwa kipindi cha miezi 12 mfululizo, pasipo kuwa na ujauzito au magonjwa yanayoathiri hedhi. Ukiingia koma hedhi kabla ya umri wa miaka 40, wasiliana na daktari kwa uchunguzi na tiba. Koma hedhi hutanguliwa mara nyingi na kukoma kwa uzalishaji wa mayai na kupoteza uwezo wa kupata ujauzito.


Hatua za kukoma kwa hedhi

 1. Kipindi kabla ya kukoma kwa hedhi- Hutokea kabla ya kufikisha umri wa miaka 40 huambatana na dalili mbalimbali

 2. Kipindi cha kuelekea koma hedhi- Kipindi hiki huambatana na dalili za kufikia mwisho wa hedhi kukoma

 3. Koma hedhi- Hiki ni kipindi cha umri wa miaka 45 hadi 55 wastani wake ni miaka 50

 4. Kipindi baada ya koma hedhi- Hiki ni kipindi baada ya hedhi kukoma na kutuoina angalau kwa miezi 12 mfululizo


Visababishi


Koma hedhi hutokea kama ovari imekoma kuzalisha mayai na hakuna homoni kukosekana kwa homon zinazosisimua ovari kuzalisha mayai hayo.


Visababishi vya komahedhi kabla ya wakati

Komahedhi kabla ya wakati huweza tokea kwenye umri wowote ule kabla ya kufikisha umri wa miaka 45 na mara nyingi hakuna sababu inayofahamika kuhusika.


Baadhi ya sababu zinazochangia kupata koma hedhi kabla ya wakati ni;


 • Matibabu ya upasuaji wa kuondoa ovari

 • Baadhi ya matibabu ya saratani ya titi

 • Matumizi ya dawa za saratani (kemotherap)

 • Matibabu ya saratani kwa njia ya mionzi

 • Kuwa na sindromu ya Down's

 • Kuwa na ugonjwa wa Addison's


Umri wa koma hedhi


Koma hedhi huweza anza taratibu kwa kipindi cha miezi kadhaa au kwa miaka kadhaa kabla ya kusimama kabisa. Unaweza kuwa na vipinid vya kutoona hedhi na kurejea kisha kukoma kabisa.


Koma hedhi hedhi asili mara nyingi hutokea kwa mwanamke anapofikisha umri wa miaka 45 hadi 55, wastani wa ukiwa miaka 51


Koma hedhi inaweza tokea kabla ya umri wa miaka 45?

Ndio koma hedhi inaweza kutokea kwa baadhi ya wanawake walio chini ya umri wa miaka 40. Tafiti zinaonyesha, mwamake 1 kati 100 hukomahedhi kabla ya kufikia umri wa miaka 40 na hii hufahamika komahedhi kabla ya wakati. Visababishi vya aina hii ya komahedhi mara nyingi huwa havifahamika lakini baadhi ya sababu zimeorodheshwa kwenye aya zinazofuata.


Dalili za koma hedhi


 • Kuongezeka kwa lehemu kwenye damu, hii humpelekea mwanamke huyu kuwa na hatari ya kupata magonjwa ya moyo

 • Mifupa kuwa dhaifu kuweza kuvunjika kwa uraisi, hii ni kutokana na hali ya kuwa na homoni kiasi kudogo cha Estrogen

 • Mfumo wa umeng’enyaji chakula kwenda taratibu na mara nyingi hupelekea kukosa choo au kupata choo kigumu

 • Kukojoa mara kwa mara kutokana na mrija wa mkojo na mfuko wa mkojo kuwa mfupi na mwembamba kutokana na upungufu wa homon Estrogen

 • Kusinyaa na kupungua umbo la ovari

 • Kusinyaa kwa mirija wa fallopio

 • Kusinyaa kwa mfuko wa uzazi

 • Kusinyaa kwa kuta za uke uke huwa na kupata hali ya akaline

 • Kusinyaa kwa maeneo ya siri ( uke na mashavu yake)

 • Kusinyaa kwa matiti na kupungua umbile au kulala

 • Ngozi ya mwili huanza kusinyaa na kutokuvutia

 • Kuongezeka kwa Uzito

 • Kupoteza nywele maeneo mbalimbali ya mwili

 • Sauti huanza kuwa ndogo

 • Kutokwa na jasho wakati wa usiku

 • Kuhisi hali ya joto, huanzia kwenye uso na ghafla husambaa kwenda kwenye shingo na mwili mzima

 • Maumiu ya kichwa yamara kwa mara

 • Mwili kuchoka

 • Kuwa na hali ya huzuni

 • Kukosa usingizi

 • Kukosa hamu ya mapenzi

 • Uke kuwa mkavu


Kumbuka

Dalili za mapema za komahedhi hutokea kabla ya miaka 40


Wakati gani wa kuonana na daktari?


Unapswa kuwasiliana na daktari wako kama utaona dalili za hedhi kabla ya kufikisha umri wa miaka 45 au dalili za komahedhi zinakusumbua kiasi cha kutoweza ishi vema.


Daktari mbali na kuthibitisha kwa dalili, atashibitisha kuwa umeingia komahedhi kwa kipimo cha kiwango cha homon kwenye damu kama komahedhi imetokea kabla ya kuingia umri wa miaka 45


Matibabu


Matibabu huhusisha tiba ya dawa za homoni ziada kwa ajili ya kupunguza dalili za koma hedhi na kuzuia mifupa kuvunjika


Dawa mchanganyiko wa Estrogen na progesterone hutolewa kwa pamoja, Estrogen endapo ikatolewa peke yake kwa mama mfuko wa uzazi huweza kupelekea kukua na kupelekea kansa ya kizazi

Estrogen peke ake hutolewa kwa kwa wanawake ambapo vizazi vyao vilikwisha kutolewa

Tiba saikolojia na kujitambua


Matibabu mengine

Zipo njia za kufanya endapo mama hataweza kupata homoni za mbadala


 • Kufanya mazoezi

 • Kula vyakula vyenye protini kwa wingi

 • Kupewa vidongr madini ya ziada ya kalisiamu

 • Kupewa vitamin D ya ziada

 • Kuacha kuvuta sigara na pombe


Madhara


Matumizi ya homoni za ziada katika kutibu dalili za komahedhu huongeza hatari ya;


 • Kupata saratani ya kizazi

 • Kupata saratani ya matiti

 • Kupata magonjwa ya moyo

 • Magonjwa ya kusahau

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

8 Oktoba 2021 04:52:43

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1.Web.Md.Menopause.https://www.webmd.com/menopause/guide/menopause-symptoms-types. Imechukuliwa 10/4/2020

2.Health.Line.Today.Menopause.https://www.healthline.com/health/menopause.Imechukuliwa 10/4/2020

3.Menopause. National Institute on Aging. http://www.nia.nih.gov/health/publication/menopause. Imechukuliwa 10.04.2020

4.Casper RF, et al. Clinical manifestations and diagnosis of menopause. https://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 10.04.2020

5.Longo DL, et al., eds. Menopause and postmenopausal hormone therapy. In: Harrison's Principles of Internal Medicine. 19th ed. New York, N.Y.: McGraw-Hill Education; 2015. http://accessmedicine.mhmedical.com. Imechukuliwa 10.04.2020

6.Nelson LM, et al. Clinical manifestation and evaluation of spontaneous primary ovarian insufficiency (premature ovarian failure). https://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 10.04.2020

7.Menopausal symptoms and complementary health practices. National Center for Complementary and Alternative Medicine. http://nccam.nih.gov/health/menopause/menopausesymptoms. Imechukuliwa 10.04.2020

8.Medical.New.Today.Menopause.https://www.medicalnewstoday.com/articles/155651.Imechukuliwa 10/4/2020

9.Dc Dutta Textbook Gynaecology ISBN 978-93-5152-068-9 written by Hiralal Konar Ukurasa wa 57-60

bottom of page