top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Adolf S, MD

9 Desemba 2020 18:11:33

Kushuka kwa kinga  mwilini
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Kushuka kwa kinga mwilini

Kushuka kwa kinga za mwili ni hali inayotokea pale endapo kinga zako za mwili zimeshuka katika kiwango ambacho kinafahamika kuwa kawaida kwa binadamu. Kushuka kwa kinga za mwili hufahamika kitiba kwa jina la immunodeficiency. Kuna aina mbili za immunodeficiency, aina ya awali na sekondari.


Makala hii imezungumzia kuhusu immunodeficiency ya awali. Kusoma kuhusu immunodeficiency ya sekondari ingia kwenye makala ndani ya tovuti hii ya ULY CLINIC.


Ni nini maana ya upungufu wa kinga wa awali

Upungufu wa kinga wa awali ni tatizo la kuzaliwa na kinga za mwili zilicho chini ya kiwango cha kawaida kwa binadamu. Kiwango cha chini cha kinga za mwili huweza kuambatana na dalili au zisiambatane na dalili. Kuonekana kwa dalili pia huweza tokea kwenye umri wowote ule. Mara nyingi kuwa na kinga za mwili za chini ya kiwango huambatana na dalili za maambukizi ya kujirudia rudia na hatari ya kupata saratani za lymphoma na magonjwa ya autoimmune.


Dalili


Mtu mwenye kinga za mwili za chini mara nyingi huambatana na dalili mbalimbali za kupata maambukizi ya kujirudia, makali au yanayodumu kwa muda mrefu. Hata hivyo mtu hupata maambukizi nyemelezi ambayo watu wenye kinga za mwili za kawaida huwa hawayapati. Dalili zingine za immunodeficiency ya awali zinahusisha;


  • Maambukizi ya kujirudia rudia ya nimoni, homa ya uti wa mgongo, masikio, ngozi na mfumo wa njia za hewa

  • Maambukizi kwenye viungo vya ndani ya mwili

  • Madhaifu ya chembe za damu kama kiwango kidogo cha chembe sahani na upungufu wa damu

  • Madhaifu katika mfumo wa umeng’enyaji chakula kama ile kichefuchefu na kuharisha

  • Kuchelewa kukua na kupata maendeleo ya ukuaji

  • Magonjwa ya autoimmune kama lupus, baridi yabisi na kisukari aina ya kwanza


Aina


Kama ilivyosemekana awali kisababishi cha immunodeficiency ya awali ni kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi wawili ambavyo vinaleta udhaifu wa uzalishaji wa kinga za mwili, aina za immunodeficiency ya awali zimegawanyika katika makundu kutokana na aina ya upungufu wa kinga hiyo mwilini; aina hizo ni


  • Upungufu wa B cell (antibody) hufahamika kwa jina jingine la Humoral immunity

  • Upungufu wa T cell hufahamika kwa jina jingine la Cellular immunity

  • Upungufu wa B naT cell hufahamika kwa jina jingine la Combined humoral and cellular immunity

  • Udhaifu wa seli za phagocytes

  • Upungufu wa Complement

  • Aina zisizofahamika


Vihatarishi


Kihatarishi cha kupata kinga za mwili ni kuwa na historia katika familia ya upungufu wa kinga mwilini


Matibabu


  • Matibabu hutegemea na aina ya kinga za mwili izlizopungua, huhusisha

  • Kupatiwa dawa za kujikinga na maambukizi ya bakteria

  • Kupewa kinga za mwili zinazoweza kusaidia mfumo wako wa kinga kuimarika mfano

  • Kuongzewa protini za kuongeza ukuaji na uzalishaji wa chembe za kinga za mwili

  • Kufanyiwa upasuaji wa kuwekewa seli zinazohusika na uzalishaji wa chembe za kinga mwilini(Stem cell) kutoka kwa mtu mwingine

  • Kubadilishiwa vinasaba vilivyo na udhaifu


Wakati gani uonane na daktari wako


Endapo wewe au ngugu anapata dalili zifuatazo ni vema ukaonana na daktari kwa uchunguzi


  • Kupata maambukizi mara kwa mara nay a kujirudia rudia

  • Endapo huponi ugonjwa hata kama ukitumia dawa


Madhara


Madhara ya kuwa na kinga za mwili cha chini


  • Maambukizi ya kujirudia

  • Madhaifu ya autoimmune

  • Kuharibika kwa moyo, maafu, mfumo wa neva na mfumo wa chakula

  • Kukua taratibu

  • Kuongezeka kwa hatari ya kupata saratani

  • Kupata maambukizi makali sana


Namna ya kujikinga


Namna ya kujikinga na madhara ya kinga za mwili za chini;


Endapo umeshapata tatizo la kinga za mwili, unaweza kufanya mambo yafuatayo ili kujikinga dhidi ya kupata maambukizi ya mara kwa mara.


  • Dhibiti msongo wa mawazo kwa kufanya yoga au kufanya vitu unavyovipenda

  • Fanya mazoezi kwa kuzingatia ushauri kutoka kwa daktari wako

  • Kula mlo kamili kutoka katika makundi matano ya chakula(soma katika makala za ulyclinic kuhusu mlo kamili)

  • Pata chanjo dhidi ya magonjwa mbalimbali, mwulize daktari wako akupe ushauri chanjo gani unaweza kuzipata.

  • Pata usingizi wa kutosha na lala masaa angalau nane kwa siku kila siku katika muda ule ule

  • Tunza kinywa na meno yako kwa kupiga mswaki mara mbili kwa siku au kila baada ya kula

  • Usikae karibu na watu wenye mafua ya virusi na maambukizi ya mfumo wa hewa

  • Zingatia usafi kwa kuosha mikono yako na sabuni baada ya kutoka chooni na kabla ya kula

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

19 Julai 2023 19:54:47

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1. Angel A. Justiz etal. Immunodeficiency. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK500027/. Imechukuliwa 8.12.2020
2. Bonilla FA. Primary immunodeficiency: Overview of management. https://www.uptodate/contents/search. Imechukuliwa 8.12.2020
3. Diagnostic and clinical care guidelines for primary immunodeficiency diseases. Immune Deficiency Foundation. https://primaryimmune.org/publication/healthcare-professionals/idf-diagnostic-clinical-care-guidelines-primary. Imechukuliwa 8.12.2020
4. General care. Immune Deficiency Foundation. http://primaryimmune.org/about-primary-immunodeficiencies/relevant-info/general-care/.Imechukuliwa 8.12.2020
5. Overview of Immunodeficiency Disorders. https://www.msdmanuals.com/professional/immunology-allergic-disorders/immunodeficiency-disorders/overview-of-immunodeficiency-disorders. Imechukuliwa 8.12.2020
6. Patient & family handbook for primary immunodeficiency diseases. Immune Di Deficiency Foundation. https://primaryimmune.org/patient-family-handbook. Imechukuliwa 8.12.2020
7. Primary immunodeficiency diseases. American Academy of Allergy, Asthma and Immunology. http://www.aaaai.org/conditions-and-treatments/primary-immunodeficiency-disease.aspx. Imechukuliwa 8.12.2020
8. Primary immunodeficiency.https://www.cdc.gov/genomics/disease/primary_immunodeficiency.htm. Imechukuliwa 8.12.2020

bottom of page