Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Peter A, MD
18 Aprili 2020 10:09:49
Kutapika
Kutapika ni kitendo cha kutoa nje ya mwili chakula au maji maji yaliyo tumboni kupitia mdomo, kitendo hiki hufanyika kwa haraka na huweza ambatana na maumivu katikati ya kifua.
Kutapika hufanyika kwa haraka na huambatana na maumivu makali au kiasi na hutanguliwa na kichefuchefu.
Kutapika ni moja kati ya njia za ulinzi wa tumbo na mwili dhidi ya sumu, hata hivyo huwa ni ishara ya hali au ugonjwa Fulani ulio mwilini. Wakati mwingine kutapika kunaweza kusiwe kunasababishwa na sababu ya hatari au kukawa na sababu ya hatari mwilini inayohitaji matibabu.
Matumizi ya dawa za kuzuia kutapika mara nyingi huwa haishauriwi kitaalmau, hii ni kwa sababu hupinga juhudi asili za kinga ya mwili kuondoa sumu mwilini. Hata hivyo baadhi ya hali na magonjwa husababisha kutapika kupita kiasi ambapo utahitaji uangalizi wa karibu wa daktari wako na matumizi ya dawa kuzuia kutapika. Usitumie dawa za kuzuia kutapika bila ushauri kutoka kwa daktari wako.
Dalili
Dalili ambazo huweza ambatana na kutapika
Maumivu ya tumbo
Kuharisha
Homa
Mapigo ya moyo kwenda kasi
Kutokwa na jasho
Kukauka kwa midomo
Kupungua kwa mkojo na kukojoa
Maumivu ya kifua
Kuzimia
Kuchanganyikiwa
Kulala sana
Kuishiwa nguvu
Kutapika damu
Visababishi
Hatua za awali za ujauzito
Msongo wa mawazo na hofu
Magonjwa ya figo
Kula sumu kwenye chakula
Maambukizi ya bakteria tumboni
Kula kupita kiasi
Mzio kutokana na harufu ya chakula au kitu chenye harufu
Shambulio la moyo
Jeraha kwenye ubongo
Uvimbe kwenye ubongo
Baadhi ya saratani
Kula sumu au pombe kupita kiasi
Homa ya safari
Matumizi ya baadhi ya dawa zenye maudhi ya kutapika
Matibabu ya kikemikali au mionzi mikali
Visabaishi vingine
Mzio wa anafailaksisi
Anoreksia nevosa
Ugonjwa wa apendeksi
Vetaigo
Bulimia nevosa
Sindromu ya kutapika
Msoongo wa mawazo
Kizunguzungu
Dayabekiti ketoasidosisi
Maambukizi ya sikio
Kukua kwa bandama(splenomegali)
Homa
Mawe kwenye kibofu cha nyongo
Kunywa sumu
Kucheua kwa tindikali za tumboni- GERD
Kuferi kwa moyo
Henia ya hayato
Kichwa maji(haidrosefalasi)
Haipathairoidizimu na haipothairoidizimu
Haipoparathairoidizimu
Isikemia ya utumbo
Kuziba kwa utumbo
Mvilio wa damu ndani ya fuvu la kichwa
Sindromu ya iritabo baweli
Intusasepsheni
Matumizi ya dawa za aspirini, NSAIDS, dawa za uzazi wa mpango, Digitalizi nakotiksi na antibayotiki
Ugonjwa wa menierezi
Meninjaitizi
Aleji kwenye maziwa
Saratani ya kongosho
Vidonda vya tumbo
Pancreataitisi
Stenosisi ya pairoriki
Saratani kwenye ubongo
Tiba mionzi
Sumu kwenye Ini
Wakati gani uonane na daktari haraka unapokuwa unatapika?
Unapaswa kumuona Daktari endapo utaona dalili zifuatazo;
Kutapika damu
Kuchanganyikiwa
Kichwa kuuma sana
Kupumua kwa kasi
Mapigo ya moyo kwenda mbio
Kuharisha sana
Matibabu
Matibabu ya kutapika hutegemea kisababishi, Mara nyingi kama dalili ya kutapika sababu yake haijulikani ni bora kutoitibu hii dalili ili kumsaidia daktarin kujua ni ugonjwa gani unapelekea dalili hii, kutumia dawa za kuzuia kutapika huficha ugonjwa.
Mgojwa anayetapika huweza kupatiwa matibabu ambayo ni;
Kuongezewa maji kupitia mishiopa ya damu
Kupewa dawa ya kuzuia kutapika kama kisababishi kinakulikana, Mfano kwa wa mama wajawazito.
Soma Zaidi kuhusu dawa za kuzuia kutapika katika Makala zetu hapa ULY CLINIC.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 20:02:52
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.Di Lorenzo C. Approach to the infant or child with nausea and vomiting. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 17/4/2020
2.Longstreth GF. Approach to the adult with nausea and vomiting. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 17/4/2020
3.Nausea and vomiting. Merck Manual Professional Version. http://www.merckmanuals.com/professional/gastrointestinal-disorders/symptoms-of-gi-disorders/nausea-and-vomiting. Imechukuliwa 17/4/2020
4.Longo DL, et al., eds. Nausea, vomiting and indigestion. In: Harrison's Principles of Internal Medicine. 19th ed. New York, N.Y.: McGraw-Hill Education; 2015. http://accessmedicine.com. Imechukuliwa 17/4/2020
5.WebMd.Vomiting.https://www.webmd.com/digestive-disorders/digestive-diseases-nausea-vomiting. Imechukuliwa 17/4/2020
6.EveryDayHealth.Vomiting.https://www.everydayhealth.com/vomiting/guide/. Imechukuliwa 17/4/2020
7.HealthLine.Vomiting.https://www.healthline.com/health/nausea-and-vomiting. Imechukuliwa 17/4/2020
8.MedcineNet.Vomiting.https://www.medicinenet.com/vomiting/symptoms.htm. Imechukuliwa 17/4/2020