top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Mangwella S, MD

19 Juni 2021 09:54:18

Kutapika nyongo kwa mjamzito
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Kutapika nyongo kwa mjamzito

Kutapika ni kitendo cha kawaida kwa wanawake wengi walio katika kipindi cha kwanza cha ujauzito (wiki 12 za mwazoni). Visababishi vya kutapika vinaweza kuwa vya kawaida au vinavyohitaji uchunguzi wa daktari.


Kutapika majimaji yenye rangi ya kijani yanayoelekea njano au kuanza na njano kisha kuelekea kijani au njano kijani huashiriaa kutapika nyongo.


Kuna sababu kadhaa zinazoweza sababisha kutapika nyongo wakati wa ujauzito, sababu kuu ikiwa ni na mabadiliko ya homoni.


Matibabu ya kutapika nyongo huelekezwa kwenye kisababishi na kubadili mtindo wa maisha.


Kwa nini?

Kisababishi halisi cha kutapika sana kipindi cha kwanza cha ujauzito hakifahamiki, baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa kuna mabadiliko chanya ya homoni yaliyo na uhusiano mkubwa sana na kutapika.


Wanawake wenye homoni ya hCG au estrogen kwa wingi kwenye damu wanaonekana kupata kichefuchefu zaifi na kutapika kuliko wenye kiwango cha chini cha homoni hizi wakilinganishwa. Hii ndio maana wanawake wenye mimba ya mapacha huwa na hatari ya kuwa na kiwango cha homoni nyingi ya hCG na kutapika zaidi.


Visababishi


Kutokana na ongezeko la kasi la kiwango cha homoni hCG na estrogen kipindi cha kwanza cha ujauzito, wiki ya 6 hadi ya 12, mabadiliko haya husababisha kichefuchefu na kutapika. Kutapika sana hutoa vitu vyote vilivyotumboni nje ya mwili na hivyo hufuatiwa na kutapika matapishi ya njano ambayo humaanisha tindikali inayokaa tumboni na kufuatiwa matapishi ya njano yanayoelekea kijani ambayo humaanisha nyongo. Hivyo kisababishi kukuu cha kutapika nyongo ni kutokuwa na chochote tumboni au tumbo wazi.


Visababishi vingine

Ugonjwa wa kucheua nyongo, ugonjwa huu hutokea sana kwa watu na huhitaji matibabu ya dawa au upasuaji. Maelezo zaidi ya dalili na matibabu ya kucheua nyongo yapo kwenye Makala nyingine ndani ya tovuti hii ya ulyclinic


Visabaishi vya nadra sana kipindi hiki ni kunywa pombe nyingi au kuchanganya pombe (kumbuka hairuhusiwi kutumia pombe wakati wa ujauzito) na kuziba kwa utumbo.


Dalili


Dalili zinazoambatana na kutapika nyongo kipindi cha ujauzito


Dalili za kutapika nyongo hutegemea umekula nini, nyongo inaweza kutanguliwa na kutapika chakula au maji uliyokunywa muda mfupi uliopita kisha kutapika majimaji ya njano na kufuatiwa na njano kijani ambayo ni nyongo. Unaweza kuanza kutapika nyongo moja kwa moja endapo imepita masaa kadhaa bila kula kitu chochote.


Mbali na dalili hizo unaweza kupata dalili za;


  • Maumivu ya tumbo

  • Kukosa hamu ya kula

  • Hisia za kuumwa

  • Kuishiwa maji

  • Ladha uchachu au metali kwenye mate


Viashiria vya hatari


Kama unatapika nyongo pamoja na dalili zifuatazo kwenye ujauzito basi tafuta msaada kutoka kwa daktari haraka;


  • Maumivu ya tumbo

  • Kushuka kwa shinikizo la damu

  • Mapigo ya moyo kwenda haraka

  • Kuanguka wakati unasimama kwa sababu ya kizunguzungu

  • Homa

  • Mtoto kuacha kucheza tumboni

  • Madhaifu yoyote ya mfumo wa fahamu

  • Kutapika kupita kiasi

  • Kuzimia


Kipindi gani katika ujauzito utegemee kutapika nyongo?


Maranyingi tegemea kupata dalili ya hutapika sana au kutapika nyongo kipindi cha kwanza cha ujauzito haswa katika wiki ya 6, ukali wa dalili huendelea kuongezeka kisha kupungua au kuisha kabisa ifikapo wiki ya 12 au 20 huisha.


Nini ufanye unapokuwa unatapika nyongo kwenye ujauzito?


Unatakiwa kufanya mabadiliko kidogo ya vitu unavyokula au kunywa ili kupunguza hisia za kichefuchefu na kutapika. Fanya mambo yafuatayo baada ya kushauriana na daktari wako;


  • Tumia vinywaji ambavyo havikuletei kichefuchefu kama vyenye tangawizi halisi.

  • Tumia vyakula na vitafunwa visivyo na mafuta kwa wingi na haswa vikavu.

  • Tumbo linapotulia, jaribu kunywa maji kidogo kidogo, mfano unaweza kunywa kwa kutumia kijiko kwa kila baada ya dakika moja ukanywa kijiko kimoja cha chakula, hii itazuia kupungukiwa maji. Usinywe maji mengi ili usivuruge tumbo na kusababisha kutapika


Baada ya kutapika nyongo nini cha kufanya?


Mara baad aya kutapika, kinywa chako kitakuwa na ladha mbaya, usipige mswaki endapo unatapika sana badala yake sukutua tu na maji kisha tema. Hii itasaidia kulinda meno yako na tindikali kali za tumboni.


Vipimo


Unapofika hospitali kwa sababu ya kutapika, daktari atakulzia maswali mbalimbali kuhusu dalili zinazoambatana na kutapika kwako kisha kushauri kufanyika kwa vipimo ili kuchunguza au kuthibitisha kile ambacho ameona kuwa ni kisababishi. Endapo kutakuwa na uhaja wa vipimo kufnayika baaddhi ya vipimo vitakavyofanyika ni;


  • Kipimo cha Ultrosound ya tumbo

  • Kipimo cha madini kwenye damu

  • Vipimo vingine vya damu na mkojo kuangalia ishara ya maambukizi


Matibabu


Matiabu ya kutapika nyongo hulenga kisababishi, kwa kuwa wanawake katika kipindi cha kwanza cha ujauzito hutapika sana kwa sababu ya mabadiliko ya homoni, matibabu hulenga kupunguza kichefuchefu na kutapika kwa kutumia dawa. Dawa zinazotumika zimendikwa sehmu nyingine kwenye Makala ya ‘dawa za kuzuia kutapika’ ndani ya tovuti ya ulyclinic.


Namna ya kujikinga na kutapika nyongo kipindi cha ujauzito


Wakati mwingi inaweza kuwa ngumu kujikinga na kutapika nyongo kwa sababu huwezi badili mabadiliko ya homoni mwilini mwako, hata hivyo unaweza fanya mambo yafuatayo kukusaidia;


  • Kula mlo kidogo wakati unataka kwenda kulala au kabla ya kuamka kitandani asubuh. Hii itazuia vipindi vingi vya kutapika na kutapika nyongo

  • Usiruke milo yako ya siku, hakikisha tumbo lako lina kitu ndani wakati wote

  • Zuia kula vyakula vyenye viungo kwa wingi maana hupelekea kichefuchefu

  • Pumzika kwa muda wa kutosha.

  • Pata muda wakutosha kupumzika

  • Dhibiti kichefuchefu kwa kushirikiana na daktari wako

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

8 Oktoba 2021 04:53:07

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

​

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1. Dehghan M, et al. Protocol for measurement of enamel loss from brushing with an anti-erosive toothpaste after an acidic episode. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/28682285/. Imechukuliwa 19.06.2021

2. Dengler R. (2018). Protein may explain morning sickness, and worse.
science.sciencemag.org/content/359/6382/1318.summary. imechukuliwa 19.06.2021

3. Morning sickness: Nausea and vomiting of pregnancy. (2020).
acog.org/womens-health/faqs/morning-sickness-nausea-and-vomiting-of-pregnancy. Imechukuliwa 19.06.2021

4. Msd manual. Nausea and vomiting during early pregnancy. https://www.msdmanuals.com/professional/gynecology-and-obstetrics/symptoms-during-pregnancy/nausea-and-vomiting-during-early-pregnancy. Imechukuliwa 19.06.2021

5. Smith JA, et al. Treatment and outcome of nausea and vomiting of pregnancy. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 19.06.20216.

6. Hinkle SN, et al. Association of nausea and vomiting during pregnancy with pregnancy loss: A secondary analysis of a randomized clinical trial. JAMA Internal Medicine. 2016;176:1621.

7. Smith JA, et al. Clinical features and evaluation of nausea and vomiting of pregnancy. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 19.06.2021

bottom of page