Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Sospeter B, MD
30 Oktoba 2021 12:02:45
Kuvimba miguu
Miguu kuvimba husababishwa na kutuama kwa maji kwenye chembe hai za miguu, huweza kusababishwa na matatizo katika mfumo wa mishipa ya damu, mirija ya mitoki au tatizo katika figo. Unaweza kuvimba miguu kwa sababu pia ya kukaa ama kusimama mda mrefu sehemu moja.
Visababishi vya kuvimba miguu
Kuna aina mbili za visabaishi, aina ya kwanza ni kutokana na kuvia kwa maji na aina ya pili kutokana na michomo kwenye chembe hai maeneo ya miguu. Maelezo zaidi yanapatikana kwenye aya zinazofuata.
Kuvimba miguu kutokana na mkusanyiko wa maji kwenye tishu za miguu
Magonjwa ya kuta za moyo
DVT
Kufeli kwa moyo
Matibabu ya dawa za homoni
Kuziba kwa mishipa ya ngiri
Kuharibika kwa mishipa midogo ya ndani ya figo
Dawa za kutuliza maumivu kama ibrupofen na naproxen
Michomo kwenye kuta za moyo
Madawa kama madawa ya kisukari na shinikizo la damu
Kusimama kwa mda mrefu, kukaa kwa mda mrefu kama kwenye ndege na gari
Magonjwa ya mishipa ya damu
Mishipa ya damu ya vein kushindwa kurudisha damu kwenye moyo
Kuvimba miguu kutokana na magonjwa ya michomo kinga
Kuvunjika kwa mfupa
Maambukizi kwenye ngozi
Gauti
Maambukizi kwenye vidonda vya miguuni
Maambukizi kwenye vijifuko vya maji katika maungio ya miguu
Misuguano ya mifupa katika maungio
Baridi yabisi
Jeraha kwenye maungio ya visigino
Matibabu ya nyumbani kwa miguu inayovimba
​
Matibabu yafuatayo yanaweza kufanywa na mtu yeyote akiwa nyumbani endapo ana tatizo la miguu kuvimba. Matibabu haya yanaweza kutumiwa tu endapo umeongea na daktari wako kwamba yapi ni yapi yanakufaa Zaidi kulingana na hali yako.
​
Mjongeo
Ukijongesha misuli kwenye maeneo ambayo yana uvimbe, mfano uvimbe kwenye kiwiko cha mguu au kwenye goti unatakiwa jongesha misuli ya miguu. Kufanyisha mazoezi miguu kwa kutembea mwendo au kukunja na kunyoosha kwa muda wa dakika 15 hadi 30 kunaweza saidia kupunguza uvimbe.
​
Kunyanyua miguu juu dhidi ya mwili
Hakikisha unanyanyua miguu yako juu ya usawa wa moyo mara kwa mara, unaweza kufanya hivi ukiwa umelala wakati wa mchana au usiku. Kuwezesha kunyanyua miguu juu, wakati umelala weka mto chini ya miguu ili miguu iwe juu Zaidi ya mwili.
​
Kukanda miguu
Kanda kwa kukamua miguu kuelekea juu kwenye magoti, tumia nguvu kidogo isipite kiasi, hii inasaidia kusukuma maji na damu yaliyozidi kuelekea kwenye.
​
Mgandamizo kwenye miguu
Unaweza tumia soksi maalumu za kugandamiza miguu yako .Soksi hizi husaidia miguu isiendelee kuvimba Zaidi na pia inapunguza uvimbe. Daktari wako atashauri matumizi ya hizi soksi na namna unavyowezazipata.
​
Kinga miguu na majeraha
Hakikisha eneo la miguu yako limekuwa safi na halijakauka, na usiliweke katika mazingira ya kupata jeraha. Ngozi ikikauka au kupata majeraha ni rahisi kupata maambukizi. Siku zote yalinde maeneo yaliyovimba kwa kuvaa vituvya kukinga kupata majeraha.
​
Punguza kiwango cha chumvi
Fuata ushauri wa dakiktari kuhusu kiwango cha chumvi unachotakiwa kutumia. Chumvi huwa na tabia ya kuhifadhi maji kwenye mwili, hivyo ukila nyingi inaweza kusababisha hali ya kuvimba ikawa mbaya Zaidi.
Wapi utapata maelezo zaidi?
Maelezo ya ziada unaweza zkuyapata kwenye makala ya kuvimbamiguu kwa mjamzito
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
30 Oktoba 2021 13:56:35
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1. Bamigboye AA, et al. Interventions for varicose veins and leg oedema in pregnancy. Cochrane Database of Systematic Reviews. http://onlinelibrary.wiley.com/wol1/doi/10.1002/14651858.CD001066.pub3/abstract. Imechukuliwa 30.10.2021
2. Benninger B, et al. Anatomical factors causing oedema of the lower limb during pregnancy. Folia Morphologica. 2013;72:67.
3. Merck Manual Professional Version. Lower-extremity edema during late pregnancy. http://www.merckmanuals.com/professional/gynecology-and-obstetrics/symptoms-during-pregnancy/lower-extremity-edema-during-late-pregnancy. Imechukuliwa 30.10.2021
4. American College of Obstetricians and Gynecologists. Frequently asked questions. Pregnancy FAQ0119. Exercise during pregnancy. http://www.acog.org/~/media/For%20Patients/faq119.pdf?dmc=1&ts=20140619T1702280658. Imechukuliwa 30.10.2021
5. Merck Manual Consumer Version. Swelling during late pregnancy. http://www.merckmanuals.com/home/women-s-health-issues/symptoms-during-pregnancy/swelling-during-late-pregnancy. Imechukuliwa 30.10.2021
6. Health and Medicine Division of the National Academies Press Water. Dietary Reference Intakes for water, pota