Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Sospeter B, MD
7 Februari 2021 13:48:16
Usingizi usioisha
Kurasa hii imezungumzia kuhusu tatitizo la usingizi kupita kiasi lenye jina la kitiba la ‘Haipasomnia’
Usingizi usioisha ni hali inayotokea kwa nadra, na hukusababishia upate usingine mara nyingi zaidi baada ya kupambazuka hata kama ulipata muda mrefu wa kulala wakati wa usiku. Kwa maana nyingine tatizo hili husababisha kulala muda mrefu wakati wa usiku au kusinzia mara kwa mara baada ya kupambazuka kusikosababishwa na kuchoka au kutopata muda wa kutosha kulala wakati wa usiku. Usingizi wa namna hii hautakufanya ujihisi na nguvu wala kutosheka kulala mara baada ya kuamka.
Usingizi usioisha unaweza kukupata muda wowote na kuleta hatari kwa mfano unaweza kutokea wakati unatembea, ukiwa unaendesha pikipiki au gari n.k.
Kumbuka
Usingizi usioisha si ugonjwa, bali ni dalili ya hali au ugonjwa unaoendelea ndani ya mwili wako unaohitaji uchunguzi ili kutambua ni nini kisababishi
Aina za usingizi usioisha
Kuna aina mbili za usingizi usioisha zinafahamika, aina ya msingi na ya sekondari ya usingizi usioisha.
Aina ya msingi ya usingizi usioisha hutokea pale endapo hakuna shida nyingine yoyote ndani ya mwili iliyofahamika baada ya kufanyiwa vipimo mbalimbali. Kisababishi cha usingizi wa awali usioisha hudhaniwa kuwa madhaifu ndani ya mfumo wa umeme au sehemu ya ubongo inayodhibiti usingizi.
Wakati huo aina ya sekondari ya usingizi uioisha ni ile ambayo kuna sababu zinazofahamika mfano tatizo la ‘sleep apnea’, majeraha ndani ya kichwa, matumizi ya pombe na madhaifu ya homoni mwilini.
Dalili
Dalili kuu za usingizi usioisha ni kupata uchovu mkali wa mwili unaodumu, kusinzia sinzia na kushindwa kuamka kwa wakati kutokana na kuwa na vipindi virefu vya kulala.
Dalili zingine
Dalili zingine zinaweza kuwa pamoja na;
Kuishiwa nguvu
Kuwa mkali
Kuwa na hofu
Kukosa hamu ya chakula
Kufikiria kwa shida au kuongea kwa shuda
Kupoteza kumbukumbu
Kutojihisi kufanya chochote
Visababishi
Visababishi vya kukosa usingizi aina ya sekondari
Magonjwa ya usingizi kama narcolepsy na sleep apnea
Kutolala vema wakati wa usiku
Kuwana uzito mkubwa kupita kiasi
Matumizi ya dawa na pombe
Majeraha ndani ya kichwa au magonjwa ya mfumo wa nevakam ugonjwa wa Parkinson's
Matumizi ya dawa jamii ya tranquilizers au antihistamines
Kuzaliwa na tatizo
Msongo wa mawazo
Vipimo
Kabla ya kufanyiwa vipimo, daktari atakuuliza maswali mbalimbali ili kufahamu shida yako, baada ya hapo anaweza kuagiza vipimo ili kutofautisha tatizo lako ni la awali au sekondari na namna ya kufanya matibabu.
Baadhi ya vipimo ambavyo unaweza agizwa fanya ni;
Kipimo cha Full blood picture
Kipimo cha CT scan ya kichwa
Kipimo cha kupima usingizi kinachoitwa polysomnography
Kipimo cha electroencephalogram (EEG)
Matibabu
Matibabu huhusisha kutibu dalili. Baadhi ya dawa ambazo utaandikiwa na daktari kutibu tatizo hili ni zipo kwenye makundi ya;
Dawa kundi la ‘stimulant’ kama amphetamine, Methylphenidate na modafinil
Dawa kundi la ‘central alpha agonists’ kama Clonidine
Dawa kundi la ‘decarboxylase inhibitor’ kama Levodopa
Dawa kundi la ‘dopamine receptor agonists’ kama Bromocriptine
Dawa kundi la Antidepressants
Dawa kundi la Monoamine oxidase inhibitors.
Kinga
Baadhi ya matatizo ya usingizi kupita kiasi hayawezi kuzuilika, hata hivyo unaweza kujikinga na vihatarishi kwa;
Kufanyamazingira unayolala kuwa rafiki
Kupunguza matumizi ya pombe na kahawa
Kuacha kutumia dawa zinazosababisha kuzinzia, kulewa
Kutofanya kazi mpaka usiku wa manane
Kuacha kula mlo mkubwa wakati wa kulala
Kutumia mlo maalumu wa kupambana na tatizo hili
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 19:54:12
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.Chervin RD. Idiopathic hypersomnia. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 06.02.2021
2.Idiopathic hypersomnia. Genetic and Rare Diseases Information Center. https://rarediseases.info.nih.gov/diseases/8737/idiopathic-hypersomnia. Imechukuliwa 06.02.2021
3.Sowa NA. Idiopathic hypersomnia and hypersomnolence disorder: A systematic review of the literature. Psychosomatics. 2016;57:152.
4.Saini P, et al. Hypersomnia evaluation, treatment and social and economic aspects. Sleep Medicine Clinics. 2017;12:47.
5.Hypersomnia Information Page. https://www.ninds.nih.gov/disorders/all-disorders/hypersomnia-information-page. Imechukuliwa 06.02.2021
6.Sleep foundation. Excessive Sleepiness. https://www.sleepfoundation.org/excessive-sleepiness. Imechukuliwa 06.02.2021
7.Sleep and Hypersomnia. https://www.webmd.com/sleep-disorders/hypersomnia. Imechukuliwa 06.02.2021