top of page

Dalili na viashiria vya magonjwa mbalimbali

Unashauriwa kufuata ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala. Bofya picha au neno soma zaidi ili kuingia kwenye makala kwa undani.

Bronkaitiz sugu

Bronkaitiz sugu

Ni aina ya COPD inayosababisha kikohozi chenye makohozi, miruzi wakati wa upumuaji, na kupumia kwa shida. Wagonjwa huonyesha ishara ya rangi ya bluu vidoleni, kifua cha pipa na uvimbe, hali inayojulikana kama 'uvimbe wa bluu'

Vidonda vya utumbo mpana

Vidonda vya utumbo mpana

Husababisha maumivu ya chini ya tumbo na kuhara mara kwa mara, mara nyingine na damu, usaha, au kamasi. Dalili zinaweza kujumuisha kichefuchefu, kupungua uzito, na homa ya vipindi.

Sindromu ya Reiter’s

Sindromu ya Reiter’s

Sindromu ya Reiter’s ni sindromu yenye staha inayowapata sana wanaume, huonekana na dalili za urethraitiz kali na hutokea wiki 1 hadi 2 baada ya kufanya ngono.

Yurethraitisi

Yurethraitisi

Urethraitis hutokana na michomo kwenye mrija wa urethra kama matokeo ya shambulio la kinga ya mwili kwenye vimelea wa maradhi walio kwenye mrija huo haswa wale wanaosababisha magonjwa ya zinaa.

Iskemia ya ateri  mesenteriki

Iskemia ya ateri mesenteriki

Ni hali hatari inayosababisha maumivu makali ya tumbo, ukakamavu, na dalili za mshtuko kama mapigo ya moyo kwenda kasi na shinikizo la chini la damu. Inapaswa kushukiwa kwa wagonjwa wazee wenye historia ya magonjwa ya moyo.

bottom of page