Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Sospeter B, MD
Dkt. Benjamin L, MD
16 Mei 2023 16:41:48
Maumivu ya tumbo la juu ya kitovu
Maumivu ya tumbo la juu ya kitovu yanaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali mwilini ambayo asili yake inaweza kuwa sehemu maumivu yalipo au sehemu nyingine mbali na maumivu hayo. Baadhi ya visababishi vinaweza kuhitaji matibabu ya haraka na vingine vinaweza kusubiria kwa muda mfupi.
Baadhi ya maumivu ya tumbo la juu ya kitovu yanaweza kuwa ya kuja na kuondoka au kudumu kwa muda mrefu.
Siku zote unapopatwa na maumivu ya tumbo la juu ya kitovu unapaswa kufahamu kisababishi na kupata matibabu sahihi. Hili linawezekana kwa kuwasiliana na daktari wako kwa vipimo, tiba na ushauri.
Katika makala hii utajifunza kuhusu visababishi vya maumivu ya tumbo la juu ya kitovu.
Â
Mambo ya kukumbuka
Katika makala hii maneno yafuatayo huwa na maana moja, maumivu ya tumbo la juu ya kitovu, maumivu ya tumbo chini ya fupa titi, maumivu ya tumbo kati ya kitovu na fupatiti.
Â
Visababishi vya maumivu ya tumbo la juu ya kitovu
 Visababishi vya maumivu ya tumbo la juu ya kitovu huwa pamoja na:
Maumivu ya via (hasa yanayotokana na magonjwa kwenye mfuko wa chakula, duodenamu, ini, tezi kongosho na via vya mfumo wa nyongo)
Vidonda vya tumbo
Homa ya tumbo
Homa ya tezi kongosho
Kupooza kwa mfuko wa chakula(tumbo)
Maumivu ya rufaa ( kutokana na tatizo kwenye mapafu au moyo)
Visababishi vya maumivu yanayotishia maisha
Visababishi vya maumnivu ya tumbo yanayoweza kupelekea kupoteza maisha ya mtu endapo asipopata maumivu ya haraka ni pamoja na:
Maumivu makali ya kuziba kwa matumbo
Kutoboka kwa via ndani ya tumbo
Kuchanika kwa bandama/ini au utumbo kutokana na ajali
Iskemia ya mezenteri
Homa kali ya tezi kongosho
Kupasuka kwa kifuko cha aota
Kuchanika kwa ujauzito ulotungwa nje ya kizazi
Infaksheni ya misuli ya moyo
Maumivu yanayotishia maisha
Maumnivu ya tumbo yanayoweza kupelekea kupoteza maisha ya mtu endapo asipopata matibabu ya haraka ni:
Maumivu makali ya kuziba kwa matumbo
Kutoboka kwa via ndani ya tumbo
Kuchanika kwa bandama/ini au utumbo kutokana na ajali
Iskemia ya mezenteri
Homa kali ya tezi kongosho
Kupasuka kwa kifuko cha aota
Kuchanika kwa ujauzito ulotungwa nje ya kizazi
Infaksheni ya misuli ya moyo
Wakati gani wa kumwona daktari?
Kama unapata maumivu ya tumbo la juu ya kitovu yanayodumu zaidi ya siku moja, unapaswa kuwasiliana na daktari wako mara moja kwa uchunguzi na tiba na ushauri.
Â
Wakati gani wa kuhofia unapopata maumivu ya tumbo la juu ya kitovu?
Endapo utapata maumivu ya tumbo la juu ya kitovu yanayoambatana na dalili zifuatazo, wasiliana na daktari mara moja:
Maumivu makali sana ya tumbo
Homa
Kichefuchefu na kutapika kusikoisha
Damu kwneye kinyesi (inaweza kuwa nyekundu au nyeusi)
Kuvimba au kuwa na maumivu ukishika tumbo
Kupungua uzito bila sababu
Manjano
Â
Makala hii imejibu
Ni nini visabaishi vya maumivu ya tumbo la juu ya kitovu?
Chanzo cha maumivu ya tumbo la juu ya kitovu?
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
11 Juni 2023 10:55:35
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1. Macaluso CR, et al. Evaluation and management of acute abdominal pain in the emergency department. Int J Gen Med. 2012;5:789–97. doi: 10.2147/IJGM.S25936.
2. Esses D, et al. Ability of CT to alter decision making in elderly patients with acute abdominal pain. Am J Emerg Med. 2004;22:270. doi: 10.1016/j.ajem.2004.04.004.
3. Lee SY, et al. Prospective comparison of helical CT of the abdomen and pelvis without and with oral contrast in assessing acute abdominal pain in adult emergency department patients. Emerg Radiol. 2006;12:150. doi: 10.1007/s10140-006-0474-z.
4. Bree RL, et al., for the Expert Panel on Gastrointestinal Imaging. American College of Radiology ACR Appropriateness Criteria. Right upper quadrant pain. http://www.acr.org/SecondaryMainMenuCategories/quality_safety/app_criteria.aspx. Imepitiwa 16.05.2023
5. Bree RL, et al. For the Expert Panel on Gastrointestinal Imaging. American College of Radiology ACR Appropriateness Criteria. Right lower quadrantpain. http://www.acr.org/SecondaryMainMenuCategories/quality_safety/app_criteria.aspx. Imepitiwa 16.05.2023
6. Levine MS, et al., for the Expert Panel on Gastrointestinal Imaging. American College of Radiology ACR Appropriateness Criteria. Left lower quadrantpain. http://www.acr.org/SecondaryMainMenuCategories/quality_safety/app_criteria.aspx. Imepitiwa 16.05.2023
7. Silen W. Cope’s early diagnosis of the acute abdomen. 21. New York: Oxford University Press; 2005. 16. Berman DA, Porter RS, Graber M. The GI cocktail is no more effective than plain liquid antacid: a randomized, double blind clinical trial. J Emerg Med. 2003;25:239. doi: 10.1016/S0736-4679(03)00196-3.
8. Chey WD, et al. American College of Gastroenterology guideline on the management of H. Pylori infection. Am J Gastroenterol. 2007;102:1808–25. doi: 10.1111/j.1572-0241.2007.01393.x.
9. Brewster GS, et al. Medical myth: a digital rectal examination should be performed on all individuals with suspected appendicitis. West J Med. 2000;173:207–8. doi: 10.1136/ewjm.173.3.207.
10. Purcell TB. Nonsurgical and extraperitoneal causes of abdominal pain. Emerg Med Clin North Am. 1989;7:721.
11. Bundy DG, et al. Does this child have appendicitis? JAMA. 2007;298:438–51. doi: 10.1001/jama.298.4.438.
12. Kessler N, et al. Appendicitis: evaluation of sensitivity, specificity, and predictive value of US, Doppler US, and laboratory findings. Radiology. 2004;230:472–8. doi: 10.1148/radiol.2302021520.
13. Chang JWY, et al. Diagnosing acute pancreatitis: amylase or lipase? Hong Kong J Emerg Med. 2011;18(1):20–5.
14. Kassahun WT, et al. Unchanged high mortality rates from acute occlusive intestinal ischemia: six year review. Langenbecks Arch Surg. 2008;393:163. doi: 10.1007/s00423-007-0263-5.
15. Miller RE, et al. The roentgenologic demonstration of tiny amounts of free intraperitoneal gas: experimental and clinical studies. AJR Am J Roentgenol. 1971;112:574–85. doi: 10.2214/ajr.112.3.574.
16. Spence SC, et al. Emergent right upper quadrant sonography. J Ultrasound Med. 2009;28:479.