top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Benjamin M, MD

Dkt. Adolf S, MD

16 Mei 2023 17:27:21

Maumivu ya tumbo la juu kulia
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Maumivu ya tumbo la juu kulia

Maumivu ya tumbo la juu kulia yanaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali mwilini ambayo asili yake inaweza kuwa sehemu maumivu yalipo au sehemu nyingine mbali na maumivu hayo. Baadhi ya visababishi vinaweza kuhitaji matibabu ya haraka na vingine vinaweza kusubiria kwa muda mfupi.


Maumivu ya tumbo la juu kulia yanaweza kuwa ya kuja na kuondoka au kudumu kwa muda mrefu.


Siku zote unapopatwa na maumivu ya tumbo la juu ya kitovu unapaswa kufahamu kisababishi na kupata matibabu sahihi. Hili linawezekana kwa kuwasiliana na daktari wako kwa vipimo, tiba na ushauri.


Katika makala hii utajifunza kuhusu visababishi vya maumivu ya tumbo la juu ya kitovu.

 

Mambo ya kukumbuka

Katika makala hii maneno yafuatayo huwa na maana moja, maumivu ya tumbo la juu kulia, maumivu ya tumbo chini ya mbavu ya kulia, maumivu ya tumbo la juu ya kitovu upande wa kulia.

 

Visababishi vya maumivu ya tumbo la juu kulia

 Visababishi vya maumivu ya tumbo la juu kulia huwa pamoja na:

  • Mawe kwenye mirija ya kupitisha nyongo

  • Homa ya kibofu cha nyongo

  • Vidonda vya tumbo

  • Homa ya tezi kongosho

  • Homa ya ini

  • Homa ya kifuko cha ini ( kutokana na PID sugu)

  • Maumivu ya rufaa ( kutokana na tatizo kwenye mapafu au moyo)

 

Wakati gani wa kumwona daktari?

 Kama unapata maumivu ya tumbo la juu kulia yanayodumu zaidi ya siku moja, unapaswa kuwasiliana na daktari wako mara moja kwa uchunguzi na tiba na ushauri.

 

Wakati gani wa kuhofia unapopata maumivu ya tumbo la juu kulia?

 Endapo utapata maumivu ya tumbo la juu kulia yanayoambatana na dalili zifuatazo, wasiliana na daktari mara moja:

  • Maumivu makali sana ya tumbo

  • Homa

  • Kichefuchefu na kutapika kusikoisha

  • Damu kwneye kinyesi (inaweza kuwa nyekundu au nyeusi)

  • Kuvimba au kuwa na maumivu ukishika tumbo

  • Kupungua uzito bila sababu

  • Manjano

 

Maumivu yanayotishia maisha

Maumnivu ya tumbo yanayoweza kupelekea kupoteza maisha ya mtu endapo asipopata matibabu ya haraka ni:

  • Maumivu makali ya kuziba kwa matumbo

  • Kutoboka kwa via ndani ya tumbo

  • Kuchanika kwa bandama/ini au utumbo kutokana na ajali

  • Iskemia ya mezenteri

  • Homa kali ya tezi kongosho

  • Kupasuka kwa kifuko cha aota

  • Kuchanika kwa ujauzito ulotungwa nje ya kizazi

  • Infaksheni ya misuli ya moyo

 

Makala hii imejibu

  •  Ni nini visabaishi vya maumivu ya tumbo la juu kulia?

  • Chanzo cha maumivu ya tumbo la juu kulia?

  • Chanzo cha maumivu ya tumbo la chini ya mbavu ya kulia

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

14 Septemba 2023 04:45:07

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

​

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1. Macaluso CR, et al. Evaluation and management of acute abdominal pain in the emergency department. Int J Gen Med. 2012;5:789–97. doi: 10.2147/IJGM.S25936.
2. Esses D, et al. Ability of CT to alter decision making in elderly patients with acute abdominal pain. Am J Emerg Med. 2004;22:270. doi: 10.1016/j.ajem.2004.04.004.
3. Lee SY, et al. Prospective comparison of helical CT of the abdomen and pelvis without and with oral contrast in assessing acute abdominal pain in adult emergency department patients. Emerg Radiol. 2006;12:150. doi: 10.1007/s10140-006-0474-z.
4. Bree RL, et al., for the Expert Panel on Gastrointestinal Imaging. American College of Radiology ACR Appropriateness Criteria. Right upper quadrant pain. http://www.acr.org/SecondaryMainMenuCategories/quality_safety/app_criteria.aspx. Imepitiwa 16.05.2023
5. Bree RL, et al. For the Expert Panel on Gastrointestinal Imaging. American College of Radiology ACR Appropriateness Criteria. Right lower quadrantpain. http://www.acr.org/SecondaryMainMenuCategories/quality_safety/app_criteria.aspx. Imepitiwa 16.05.2023
6. Levine MS, et al., for the Expert Panel on Gastrointestinal Imaging. American College of Radiology ACR Appropriateness Criteria. Left lower quadrantpain. http://www.acr.org/SecondaryMainMenuCategories/quality_safety/app_criteria.aspx. Imepitiwa 16.05.2023
7. Silen W. Cope’s early diagnosis of the acute abdomen. 21. New York: Oxford University Press; 2005. 16. Berman DA, Porter RS, Graber M. The GI cocktail is no more effective than plain liquid antacid: a randomized, double blind clinical trial. J Emerg Med. 2003;25:239. doi: 10.1016/S0736-4679(03)00196-3.
8. Chey WD, et al. American College of Gastroenterology guideline on the management of H. Pylori infection. Am J Gastroenterol. 2007;102:1808–25. doi: 10.1111/j.1572-0241.2007.01393.x.
9. Brewster GS, et al. Medical myth: a digital rectal examination should be performed on all individuals with suspected appendicitis. West J Med. 2000;173:207–8. doi: 10.1136/ewjm.173.3.207.
10. Purcell TB. Nonsurgical and extraperitoneal causes of abdominal pain. Emerg Med Clin North Am. 1989;7:721.
11. Bundy DG, et al. Does this child have appendicitis? JAMA. 2007;298:438–51. doi: 10.1001/jama.298.4.438.
12. Kessler N, et al. Appendicitis: evaluation of sensitivity, specificity, and predictive value of US, Doppler US, and laboratory findings. Radiology. 2004;230:472–8. doi: 10.1148/radiol.2302021520.
13. Chang JWY, et al. Diagnosing acute pancreatitis: amylase or lipase? Hong Kong J Emerg Med. 2011;18(1):20–5.
14. Kassahun WT, et al. Unchanged high mortality rates from acute occlusive intestinal ischemia: six year review. Langenbecks Arch Surg. 2008;393:163. doi: 10.1007/s00423-007-0263-5.
15. Miller RE, et al. The roentgenologic demonstration of tiny amounts of free intraperitoneal gas: experimental and clinical studies. AJR Am J Roentgenol. 1971;112:574–85. doi: 10.2214/ajr.112.3.574.
16. Spence SC, et al. Emergent right upper quadrant sonography. J Ultrasound Med. 2009;28:479.

bottom of page