top of page

Eucalyptus globulus

Imeandikwa na:

Dkt. Benjamin L, MD

5 Agosti 2021 09:28:31

Utangulizi

Ni mmea wenye asili ya Australia hata hivyo hupatikana sehemu nyingi za ukanda wa joto barani Afrika. Huwa na uwezo wa asili kutibu kutibu kikohozi, bronkaitizi, nimonia, UTI, homa, kiungulia, mapigo ya moyo kwenda kasi na dalili za koma hedhi. Kwa Tanzania, Eucalyptus globulus hufahamika kama Mkaratusi.

Sifa za mmea Eucalyptus globulus

• Combretum glutinosum mti wake huwa wa kijani mwaka mzima na hurefuka urefu kufikia mita 60 hadi zaidi ya 99.
• Baadhi ya miti huwa na shina la pekee na baadhi huwa na mashina makubwa sana
• Mizizi yake huwa na rangi ya bluu
• Shina la mti wake na mizizi huwa na tezi za mafuta
• Huwa na sifa ya kubadili mwonekano kutokana na umri wake
• Maua yake huwa makavu na umbo la koni na magumu
• Matunda yake pia huwa magumu

Uwezo wa Eucalyptus globulus kwenye tiba

Eucalyptus globulus hutumika kama dawa ya kutibu;
• Bronkaitizi
• Kikohozi
• Nimonia
• Maambukizi kwenye mapafu
• Mafua ya virusi
• Homa
• UTI
• Kiungulia cha kutojongea kwa misuli ya tumbo
• Koo linalouma
• Dalili za koma hedhi
• Mapigo ya moyo kwenda mbio

Matumizi ya nje ya mwili

• Moshi wa majani au mafuta ya Eucalyptus globulus huwa na uwezo wa
• Kuua mbu ndani ya nyumba
• Kuondoa virusi kwenye hewa
• Kufungua njia ya hewa kwa wagonjwa wa asthma, wenye michomo kinga ya sainazi,
• Kutibu Baridi yabisi
• Kutibu Kipanda uso

Mtumizi ya Eucalyptus globulus kwenye tiba asili

Kutibu bronkaitiz

Andaa infusheni ya majani matatu hadi manne kwenye maji yaliyochemka kisha kunywa vikombe vitatu kama chai.

Kwa matibabu ya mafua ya virusi, michomo kinga kwenye sainaz, kutokwa na mafua, tia matone matatu hadi manne ya mafuta yake kwenye bakuli kubwa la maji yaliyochemshwa na kutoa mvuke kisha vuta hewa ya mvuke inayotoka.( Jifukize).

Kwa matibabu ya kuziba kwa njia ya hewa

Chukua tinkcha kijiko kimoja cha chai kwenye mililita 100 za maji kisha kunywa mara mbili kwa siku. (Tumia tinkcha iliyoandaliwa kwa kutumia jani moja na asilimia 50 ya kileo kwa muda wa wiki moja).

Tahadhali kwa watumiaji wa Eucalyptus globulus

Matumizi ya ndani ya mafuta ya Eucalyptus globulus yanahitaji uangalizi maalumu kwa sababu endapo yatatumiwa kwa muda mrefu hupelekea figo kushindwa kufanya kazi.

Wagonjwa wenye figo zilizoferi hawapaswi kutumia kwa kunywa mafuta ya Eucalyptus globulus

Bakteria wanaouliwa na mafuta ya Eucalyptus globulus

Tafiti zimethibitisha kuwa, mafuta ya maua ya Eucalyptus globulus huwa na uwezo wa kuua bakteria wafuatao;

• Pseudomonas aerugenosa
• Staphylococcus aureus
• Bacillus subtilis
• Escherichia coli
• Listeria innocua

Namna ya kuandaa aina mbalimbali za dawa kutoka kwenye mmea

Namna ya kuandaa infusheni ya dawa asilia

Infusheni huandaliwa kwa kuzamisha sehemu ya mmea unayotaka kutumia kama dawa kwenye kiasi cha maji yaliyochemka. Baada ya kuzamisha kwenye maji yaliyochemka, maji hayo huchujwa baada ya dakika 15. Dozi ya dawa inayotakiwa kuandaliwa kwa wastani huwa ni gramu 1 kwa kila mililita 10 za maji.

Kuna dawa nyingi asilia zimeshatengenezwa na kufungwa kwenye vifungashio vya karatasi ambapo unaweza kutumia kirahisi kama majani ya chai ya kuchovywa. Dawa kwenye fomu hiyo zitapunguza muda wa kuandaa.

Namna ya kuandaa dikokshen ya dawa asilia

Dikokshen hutumika kuvuna kiini cha dawa ambacho hakiathiriwi na joto.

Ili kuandaa dikokshen ya dawa, chemsha magome au mizizi ya mmea kwa muda wa dakika 15 hadi 60 (hutegemea aina ya mmea au kiini cha dawa), kisha pooza na ongeza maji ya baridi ili kutengeneza kiasi cha dawa na wingi wa kiini unachohitaji.

Endapo dawa inatakiwa kuchemka kwa muda mrefu, unatakiwa ongezea kiasi cha maji yaliyopotea ili dawa isiungue.

Dozi ya dikoksheni ni sawa na infusheni yaani gramu moja ya mmea kwa mililita 10 za maji isipokuwa endapo dawa ina uteute mwingi, gramu moja inatakiwa kuchanganywa na mililita 20 za maji.

 

Namna ya kuandaa mmengenyo wa dawa

 

Kuandaa mmeng’enyo wa dawa kwa njia hii unatakiwa weka dawa yako kwenye chombo kisha ongeza maji yenye joto linalotakiwa, mara nyingi joto linatakiwa kuwa kati ya nyuzi za sentigrade 35 hadi 40 ikitegemea aina ya dawa. Lengo kuu la kuzingatia joto ni kutoharibu kiini cha dawa ambacho kinategemea joto.

Namna ya kuandaa masalesheni ya dawa

 

Ili kuandaa masalesheni ya dawa, saga au katakata dawa kwenye vipande vidodo vidogo sana kisha weka kwenye jaa ya kioo yenye kimiminika cha kufyonza dawa. Funika mchanganyiko na acha kwa muda wa siku tatu au zaidi kwenye joto la ndani ya nyumba.Baada ya kutimia kwa siku tatu, tikisa kwa nguvu mara nyingi ili dawa iingie kwenye kimiminika. Baada ya hapo chuja dawa na kamua unga au vipande ili dawa yote itoke. Baada ya hapo unaweza kuchuja dawa kwa ajili ya matumizi au kuifanyia dekatensheni ili kupata kiini safi cha dawa.

Namna ya kuandaa pakolesheni ya dawa

 

Hii ni njia maarufu ya kuandaa tinkcha ya dawa au kufyonza dawa kutoka kwenye kimiminika.  Njia hii inahitaji chombo maalumu chenye jina la pakoleta na unatakiwa kuwa mtaalamu zaidi kuandaa dawa kwa njia hii. Soma zaidi maelezo kwa kutumia linki chini ya tovuti hii.

 

Namna ya kuandaa dawa ya kufyonza kwa kimiminika

Njia hii huandaa dawa kutoka kwenye kimiminika chenye dawa au tishu za mnyama kwa kufyonzwa dawa hiyo kwa kutumia kimiminika kingine haswa pombe aina ya ehthanol  au maji.

 

Kiasi cha pombe na maji yanayowekwa hutegemea aina ya dawa. Njia hii inahitaji uwe mtaalamu wa kuandaa dawa, unaweza kujifunza zaidi namna ya kuandaa dawa kwa njia hii kupitia linki chini ya tovuti hii au tumia dawa ambazo tayari zimekwisha andaliwa.

Namna ya kuandaa tinkcha ya dawa

 

Tinkcha ya dawa huandaliwa kwa kufanya masalesheni au pakolesheni ya dawa kwa kutumia kimiminika cha pombe tu. Njia hii ni nzuri ya kuvuna kiwango cha kiini unachotaka kutoka kwenye mimea au mnyama. Soma zaidi kuhusu njia hii kupitia rejea chini ya Makala hii.

KUMBUKA:

 

Kama kuna haja ya kuchemsha dawa, hakikisha unatumia chomo kilichotengenezwa na udongo au sufuria za stainless steel na usifunike wakati wa kuchemsha ili kutoa sumu na kutobadili kiini cha dawa.

 

Usitumie dawa zaidi moja na kutibu tatizo moja au mawili tofauti ili kuepuka madhara na mwingiliano

Endapo unatumia dawa za hospitali, wasilina na daktari wako kukushauri ili kuepuka mwingiliano wa dawa na madhara yanayoweza kutokea.

ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute msaada kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba kupitia kitufe cha 'Pata tiba' au 'Mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

26 Agosti 2021 18:33:18

Rejea za mada hii;

1. Eucalyptus globulus. https://www.gbif.org/species/3176787. Imechukuliwa 05.08.2021

2. Sonam Chouhan, et al. Antimicrobial Activity of Some Essential Oils—Present Status and Future Perspectives. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5622393/. Imechukuliwa 05.08.2021

3. Si Saida Z.B, et al. Essential oils composition, antibacterial and antioxidant activities of hydro distillated extract of Eucalyptus globulus fruits. Ind. Crops Prod. 2016;89:167–175. doi: 10.1016/j.indcrop.2016.05.018. Imechukuliwa 05.08.2021

4. ZakiaBey-Ould Si Said, et al. Essential oils composition, antibacterial and antioxidant activities of hydrodistillated extract of Eucalyptus globulus fruits. https://www.sciencedirect.com/science/article/abs/pii/S0926669016303351. Imechukuliwa 05.08.2021

5. Infusion methods. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/infusion/#. Imechukuliwa 27.06.2021

6. Decoction extraction. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/decoction/. Imechukuliwa 27.06.2021

7. Extraction methods digestion. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/digestion/. Imechukuliwa 27.06.2021

8. Fluid extract. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extracts/fluid-extract/. Imechukuliwa 27.06.2021

9. Tincture. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extracts/tincture/. Imechukuliwa 27.06.2021

10. Perolation. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/percolation/. Imechukuliwa 27.06.2021

11. Maceration. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/maceration/. Imechukuliwa 27.06.2021

bottom of page