Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
Dawa za vidonda kwenye ulimi
5 Novemba 2021 09:53:43
Vidonda kwenye kinywa kwa jina jingine hufahamika kama vidonda vya kanka, huwa ni vidonda vidogo vinavyouma, hutokea kwenye sakafu ya fizi.
Vidonda hivi husababisha usumbufu wakati wa kula na kutafuna kwani huuma sana wakati huu.
Dawa na mambo unayoweza kufanya kutibu vidonda kinywani ni pamoja na;
​
Kutumia maji yenye baking soda kusukutua kinywa chako mara mbili hadi tatu kwa siku
Kuweka uji wa magniziamu kwenye kidonda
Kufunika/kupaka uji wa baking soda kwenye kidonda
Kutumia benzocaine (tafuta ushauri wa daktari kwanza) kupunguza maumivu
Kutumia barafu kwa kuilamba au kuiweka karibu na kidond kupunguza maumivu
Dawa jamii ya steroid kupunguza uvimbe na maumivu
Kutumia dawa ya mswaki
Matumizi ya viinirishe kama foliki acid
Matumizi ya vitamin B6 na 12
Matumizi ya madini ya zinki
Matumizi ya dawa asilia kama majani ya chai yam mea wa chamomile
​
Soma zaidi kuhusu vidonda kwenye ulimi kwa kubonyeza hapa