Imeandikwa na daktari wa uly clinic
​
Maumivu ya ulimi
​
Utangulizi
​
Maumivu ya ulimi yanaweza kusababishwa na hali au matatizo mbalimbali, maumivu yanaweza kuwa ya aina tofauti mfano kuhisi ulimi unawaka moto au kuchoma choma unapokuwa unakula au kunywa, mara unapoamka tu na yana kaa siku nzima, maumivu ya kuja na kuondoka au maumivu hayo kuwepo muda wote na pengine kudumu kwa miaka kadhaa.
​
Kwa kawaida maumivu kwenye ulimi yanaweza kusababishwa na maambukizi au majeraha kwenye ulimi. Majeraha yanaweza kutokana na mtu kujing’ata au kuumizwa na kitu. Wakati mwingine si rahisi kujua kama umepata jeraha kwenye ulimi. Majeraha ya ulimi yanaweza kupona baada ya siku kadhaa na hali ya maumivu kupotea.
​
Kwenye mada hii utasoma kuhusu, vidonda kwenye ulimi na ulimi kuwaka moto
​
Vidonda kwenye ulimi
​
Vidonda kwenye ulimi huweza kuonekana Kama vijishimo vidogo vyenye rangi nyeupe au njano kwenye ulimi au kwenye fizi chini kidogo ya meno. Vidonda hivi huitwa canker, huwa haviambukizwi na mara nyingi husabaishwa na vitu tunavyotumia kila siku kama kemikali kwenye dawa za miswaki, dawa za kuosha mdomo, mzio wa chakula, au upungufu wa vitamin aina fulani mwilini. Wakati mwingine hakuna kisababishi kinachojulikana kusababisha vidonda hivi.
Visababishi vingine vya maumivu ya ulimi huwa pamoja na
-
Saratani
-
Upungufu wa damu
-
Maambukizi ya virusi vya Herpes
-
Kuvaa vidani kwenye ulimi
-
Matatizo ya mishipa ya fahamu
​
Endelea kusoma zaidi kuhusu kuhusu
​
Endapo umesoma na kuona una tatio hili ni vema ukawasiliana na daktari wako kwa uchunguzi na tiba
​
Unaweza pata ushauri na tiba kutoka kwa daktari wa ulyclinic kwa kubonyeza hapa au piga namba za simu chini ya tovuti hii
​
Bonyeza kusoma zaidi kuhusu Ulimi jiografia/ramani, pellagra, sindromu ya cowdens, leukoplakia, sindrome ya kuungua kwa Kinywa/mdomo, Ulimi ulio pasuka na kuchanika chanika
​
Imeboreshwa mara ya mwisho 14.04. 2020