top of page

Dawa za kutibu arithmia

​

Matibabu ya arithmia yanategemea aina ya arithimia aliyonayo mgonjwa, na kipimo cha elekrokadiografi. Visababishi vinahitaji kutibiwa ipasavyo mfano moyo kuferi n.k

​

Mapigo ya Ektopik

Kama mapigo ya Ektopiki yameanza yenyewe na moyo wamgonjwa hauna shida, matibabu mara nyingi hayatahitajiki, mtulize mgonjwa mwambie kwamba atakuwa sawa.

Kama hali itakuwa mbaya basi matibabu ya dawa jamii ya beta bloka wakati mwingine husaidia na huwa salama kuliko dawa zingine.

​

Fibrilesheni ya atria

Matibabu hulenga kupunguza dalili na kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza kama vile kiharusi.

Wagonjwa wote wenye fibrilesheni ya atria wanatakiwa kuchunguzwa kama wapo na hatari ya kupata kiharusi na thromboembolizimu. Fibrilesheni ya atria inaweza kutibiwa kwa kudhibiti mapigo ya ventriko au kurejesha na kustahimilisha rizimu za sainaz.

Katika hatua zozote zile za tiba, endapo matibabu yamefeli kudhibiti dalili, au dalili zinarejea baada ya kadiovesheni na matibabu ya kibobezi unahitaji kumpeleka mgonjwa kupata matibabu ya kibobezi zaidi ndani ya wiki 4.

​

Kama matibabu ya dawa yamefeli kudhibiti dalili au fibrilesheni ya atria au hayafai, mikakati ya tiba ya ablashen inatakiwa kufikiriwa. Rejea kujua vihatarishi vya, kiharusi, kutokwa na damu na matumizi ya dawa za antikoagulashen kila mwaka kwa kila mgonjwa mwenye fibrilesheni ya atria

​

Dawa za kutibu arithmia (anti-arithmia)

Dawa za anti arithmia zinaweza kugawanywa kwenye kundi  kulingana na tatizo halisi la arithmia mfano zile zinazofanya kazi kwenye arithmia ya

  • Supraventrikula mfano verapamil hydrochloride

  • Supraventrikula na ventrikula mfano amiodarone hydrochloride

  • Ventrikula mfano lidocaine

 

Na kundi la dawa kulingana na madhara kwenye tabia ya umeme ya seli za mayokadia wakati wa ufanyaji kazi wake. Mgawanyo huu hauzingatii hali halisi ya moyo. Makundi hayo ni pamoja na dawa za;

​

bottom of page