Mwanshishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
29 Julai 2020 19:55:37

Econazole ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Ecoza.
Fomu ya dawa Econazole
Econazole hupatikana kwenye fomu ya krimu yenye ujazo mbalimbali na asilimia 1 ya kiini cha dawa
Namna Econazole inavyofanya kazi ili kutibu fangasi
Dawa hii ya Sulconazole hufanya kazi zake kwa kuharibu ukuta wa seli ya fangasi. Sulconazole na aina nyingine za dawa ya fangasi hufanya kazi kwa kuzuia utengenezaji wa ergosteroli ambayo huhitajika kwa ajili ya kutengeneza ukuta wa seli ya fangasi. Egosteroli huwa muhimu sana kwenye seli ya fangasi. Kama ergosteroli haitengenezwi, seli ya fangasi hushindwa kutengeneza ukuta wake wan je na hufa.
Dawa zingine kundi moja na Econazole
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo; • Amphotericin B • Butoconazole • Capsofungin • Ciclopiro • Fluconazole • Flucytosine • Griseofulvin • Itraconazole • Ketoconazole • Miconazole • Naftifine hydrochloride • Nystatin • Oxiconazole nitrate • Sulconazole nitrate • Terbinifine • Terconazole • Tioconazole • Tolnaftate • Voriconazole
Kazi za Econazole
Hutumika kwenye matibabu ya maradhi ya fangasi waliyo kwenye ngozi na waliyosambaa sehemu mbalimbali za mwili.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Econazole
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi
Matumizi ya Econazole kipindi cha ujauzito
Inaweza kutumika endapo faida ni kubwa kuriko madhara yanayoweza kujitokeza
Matumizi Econazole kwa mama mjamzito
Dawa hii hushauriwa kutumika endapo faida zinazidi madhara au pale ambapo hamna dawa nyingne mbadala wakati wa kipindi cha ujauzito.
Matumizi wakati wa kunyonyesha
Takwimu hazionyeshi kuwa kuna huwezekano wa hii dawa kuingia au hapana kwenye maziwa ya mtoto hivyo inashauriwa itumike kwa wamama wanaonyonyesha kwa huangalifu mkubwa.
Maudhi ya Econazole
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni; • Kuwashwa mwilini • Kuhisi kuungua mwilini
Je endapo utasahau dozi yako ya Econazole ufanyaje?
Endapo umesahau kutumia dozi yako, kunywa au paka mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:55:27
Rejea za mada hii:-