Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
4 Aprili 2020 17:45:07
Abacavir (ABC)
Abacavir ni dawa mojawapo ya kudhoofisha makali ya Virusi vya UKIMWI(ART) na ipo kwenye kundi la dawa zinazoitwa NRTIs. Dawa hii haitumiki kama yenyewe, huchanganywa na dawa zingine za ART kudhibiti makali ya VVU. Kundi la dawa za NRTIs hufanya kazi ya kupunguza makali ya VVU kwa kuzuia RNA ya kirusi kujitengenezea DNA. Ili RNA itengeneze DNA inahitaji kimeng’enya kinachoitwa Reverse Transcriptase, abacavir huzuia kimeng’enya hiki na hivyo kirusi kushindwa kujuzalia.
Rangi na Fomu ya Abacavir (ABC)
Dawa hii hupatikana katika fomu ya kidonge na kimiminika
Rangi ya kidonge hutofautina kulingana na kampuni, inaweza kuwa nyeupe, njano mpauko, n.k Huweza kutumika hata pasipo chakula na kidonge huwa chenye miligramu 300, dawa ya maji huwa na miligramu 20 kwa kila mililita moja
Dawa kundi moja na Abacavir
Lamivudine (3TC)
Emtricitabine (FTC)
Zidovudine (AZT)
Abacavir hutibu nini?
Hutumika pamoja na dawa zingine katika kuthibiti virusi vya UKIMWI. Abacavir itatumika endapo
imeungana na dawa zifuatazo ikiwemo yenyewe.
Abacavir (ABC) +Lamivudine (3TC) +Dolutegravir (DTG) kwa kifupi TRIUMEQ
Abacavir/Lamivudine
Abacavir, Lamivudine, Tenofovir
Abacavir hufahamika kwa jina jingine la Ziagen
Dozi ya Abacavir (ABC)
Mgonjwa anapaswa kutumia dawa hii kama ambavyo atakavyoelekezwa na Daktari.
Dawa zisizopaswa kutumika na Abacavir (ABC)
Emtricitabine
Ganciclovir
Ribavirin
Tipranavir
Zidovudine
Atanazavir
Didanosine
Methadone
Orlistat
Ethanol
Elvitegravir/cobicistat/emtricitabine/tenofovir
Abacavir ikitumiwa na dawa zifuatazo, mgonjwa anatakiwa kuwa chini ya uangalizi:
Fosamprenavir
Indinavir
Lamivudine
Methadone
Nelfinavir
Nevirapine
Atazanavir
Cabozantinib
Saquinavir
Stavudine
Tenofovir df
Tipranavir
Zidovudine
Didanosine
Efavirenz
Emtricitabine
Enfuvirtide
Orlistat
Ritonavir
Wagonjwa wasiopaswa kutumia abacavir
Mwenye historia ya mzio wa dawa hii
Wenye matatizo ya ini
Tahadhari kwa mtumiaji
Tahadhari inapaswa kuchukuliwa kwa;
Waliovimba ini
Wenye magonjwa mengine yanayoharibu kinga ya mwili kama ugonjwa wa Graves
Matumizi kwa mama mjamzito
Tafiti hazijathibitishwa kwamba ni kwa kiasi gani madhara kwa mtoto yanaweza kutokea ikiwa pamoja na matatizo katika uumbaji wa mtoto akiwa tumboni mwa mama.
Matumizi kwa mama anayenyonyesha
Mama mwenye Maambukizi ya HIV hapaswi kunyonyesha wakati wa miezi 6 yote hata hivyo haina madhara endapo itapita katika maziwa
Maudhi ya abacavir
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hi ni pamoja na:
Uchovu wa mwili
Homa
Maumivu ya misuli
Maumivu ya kichwa
Vipele
Kichefuchefu
Kutapika
Mzio
Kuwa na woga na hofu
kushuka kwa shinikizo la damu
Konstipesheni
Kukosa usingizi(insomnia)
Upungufu wa damu
Maumivu ya tumbo
Kukohoa
Anoreksia
Je kama umesahau dozi yako ya Abacavir (ABC) ufanyaje ?
Dawa hii hutumika kwa mchanganyiko pamoja na dawa zingine za kuthibiti VVU, endapo utasahau kunywa dozi yako, unapaswa kunywa na Kuendelea na muda huo siku inayofuata.
Lakini ukikumbuka kunywa baada ya masaa 24 kupita, kunywa dozi inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari na achana na dozi uliyosahau.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:50:37
Rejea za mada hii:-