Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
28 Juni 2020, 19:09:32

Aliskiren
Aliskiren ni aina ya dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu Iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa Renin inhibita. Dawa hii iliyo maarufu kwa jina la Tekturna huwa na rangi ya pinki au nyekundu isiyokolea hata hivyo mara nyingi hutegemea aina ya kiwanda kinachotengeneza dawa.
Aliskiren inapaswa kutumiwa pamoja na chakula mara mbili kwa siku kama utakavyoelekezwa na kushauriwa na daktari.
Fomu na uzito wa dawa
Vidonge
• 150 Mg
• 300 Mg
Tembe
37.5 Mg
Namna dawa inavyofanya kazi;
Dawa jamii ya Renin Inhibita ikiwa pamoja na Aliskiren hufanya kazi zifuatazo ili kushusha shinikizo la damu;
Dawa hii huzuia kubadilishwa kwa kiungo muhimu cha angiotensinogen kwenda homoni ya Angiotensin I. Kupungua kwa homoni ya angiotensin I husababisha kupungua kiasi cha angiotensin II. Homoni ya angiotensin II hufanya kazi ya kuchochea mishipa ya damu kupunguza kioenyo hivyo kuleta shinikizo la damu. Kwa dawa hii kuzuia shughuli hizo, shinikizo lla damu hupungua mara mtu anapotumia dawa hii.
Dawa zilizo kundi moja
Remikiren
Kazi ya dawa
Hutumika kushusha shinikizo la juu la damu
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Azilsartan
Benazepril
Candesartan
Captopril
Enalapril
Eprosartan
fosinopril
Irrbesartan
Lisinopril
Losartan
Moexipril
Olmesartan
Perindopril
Quinapril
Ramipril
Telmisartan
Trandolapril
Valsartan
Wagonjwa wasiopaswa kuitumia
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii dawa zingine jamii ya dawa za Renin Inhibita
Tahadhari ya dawa hii
Huweza kumpelekea mtu kupata aleji na kuweza kuvimba uso,ulimi na mdomo
Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wenye shida ya figo
Matumizi kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Kwa mama mjamzito katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito itumike kwa tahadhari endapo faida ni nyingi kuzidi hatari kwa kichanga tumboni
Matumizi kwa mama anayenyonyesha
Haipaswi kutumika kwa mama anayenyonyesha kwa sababu haijulikani kama hutolewa kwenye maziwa baada ya kutumia dawa hii
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;
Kuharisha
Kukohoa
Kutokwa na vipele kwenye ngozi
Haipakalemia
Kuvimba
Maumumivu ya kichwa
Nusu maisha na utoaji wa dawa mwilini
Kiwango cha juu cha dawa kwenye damu hufikiwa kwa saa 1 hadi masaa 3 na nusu maisha ya dawa mwilini ni masaa 24
Mabaki yake hutolewa kwa njia ya Mkojo kwa asilimia 23
Je kama umesahau dozi yako ufanyaje?
Kama umesahau dozi yako ya dawa unapaswa kunywa mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:55:27
Rejea za mada hii:-