Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
18 Aprili 2020, 20:04:35

Alogliptin
Alogliptin ni dawa ya inayotumika katika tiba ya ugonjwa wa kisukari aina ya pili, ipo kwenye kundi la dawa linaloitwa dipeptidyl peptidase-4 (DPP-4) na hufahamika kwa jina jingine la Nesina.
Dawa hii ni ya kumeza, hutuka baada ya kula chakula au kunywa wakati unakula chakula.
Rangi ya Alogliptin
Rangi ya dawa mara nyingi huwa nyeupe, hata hivyo mara nyingi hutegemea rangi iliyopendekezwa na kiwanda.
Dawa zilizokundi moja na Alogliptin
Dawa zingine ambazo zipo kwenye kundi moja na Alogliptin ni;
Saxagliptin
Sitagliptin
Linagliptin
Vildagliptin
Jinsi Alogliptin inavyofanya kazi
Hufanya kazi kwa kuongeza kiasi cha homoni za kimetaboli zinazoitwa inkretin ambazo huthibiti kiwango cha glukosi kwenye damu kwa kuchochea kuzalishwa zaidi kwa homoni ya Insulin, hasa baada ya kula
Hupunguza kiasi cha sukari kinazalishwa na ini kisha kuingia kwenye damu.
Kazi za Alogliptin
Hutumika kwenye matibabu ya kisukari kwa wagonjwa wenye kisukari aina ya pili.
Dawa usizopaswa kutumia pamoja na Alogliptin
Alogliptin inapotumika pamoja na dawa zifuatazo mgonjwa anapaswa kufuatiliwa kwa ukaribu sana;
Benazepril
Captopril
Chlorpropamide
Dulaglutide
Glimepiride
Glipizide
Glyburide
Insulin aspart
Insulin degludec
Insulin detemir
Insulin glargine
Insulin glulisine
Insulin lispro
Nateglinide
Repaglinide
Tolazamide
Tolbutamide
Wagonjwa wsiopaswa kutumia Alogliptin
Wagonjwa wenye mzio na dawa hii
Tahadhari ya Alogliptin
Huweza kupelekea Ini kushindwa kufanya kazi
Husababisha pankriataitizi
Inapaswa kusimamishwa endapo italeta mzio wa anafailatiki kwa mgonjwa
Matumizi ya Alogliptin Kwa mama
Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa mama mjamzito
Hakuna athari zozote kwa mtoto ikitumika kwa mama anayenyonyesha.
Maudhi ya Alogliptin
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa ni;
Kushuka kwa glukosi hasa ikitumika pamoja na Insulin
Nasofarinjaitizi
Maumivu ya kichwa
Maambukizi kwenye mfumo wa juu wa upumuaji
Pankriataitizi
Je ekama umesahau dozi ya Alogliptin ufanyeje?
Kama umesahau kutumia dozi yako, Tumia dawa mara utakapokumbuka isipokuwa endapo muda wa dozi ingine umefika. Kama muda wa dozi ingine umefika ruka dozi hii uliyosahau na endelea kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:51:23
Rejea za mada hii:-