Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
24 Juni 2021, 07:10:07

ALU
ALU ni dawa yenye maana ya artemether/lumefantrine, mchanganyiko wa dawa mbili ya artemether na lumefantrine iliyo kwenye kundi la dawa za kutibu malaria.
Majina mengine ya ALU
Majina mengine ya dawa ya ALU ni;
Dawa ya Coartem
Dawa ya mseto
Dozi na fomu ya ALU
ALU hupatikana katika fomu ya kidonge chenye uzito wa miligramu;
20/120
40/480
Namna ALU inavyofanya kazi yake
Artemether na lumefantrine hufanya kazi yake ya kutibu malaria kwa kuzuia uzalishaji wa DNA ya vidudu vya malari na protini zake.
Dawa zilizo kundi moja na ALU
Dawa zilizo kundi moja na ALU yaani dawa za kutibu malaria ni;
Artemether/Lumefantrine
Artesunate
Atovaquone
Atovaquone/Proguanil
Chloroquine
Chloroquine Phosphate
Daraprim
Fansidar
Hydroxychloroquine Sulfate
Malarone
Mefloquine
Primaquine
Proguanil
Pyrimethamine
Pyrimethamine/Sulfadoxine
Pyrimethamine-Sulfadoxine
Quinaglute
Quinidex
Quinidine
Quinidine Gluconate
Quinine
Tafenoquine
Kazi ya dawa ALU
Hutibu malaria isiyokali
Usitumie ALU wakati gani?
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wenye Mzio na dawa hii
Tahadhari kwa watumiaji wa ALU
Haipaswi kutumika kwa wagonjwa wenye malaria kali
Haikingi malaria
Huweza kupunguza ufanisi wa dawa za uzazi wa mpango
Kama mgonjwa akirudia kutapika dawa tumia dawa aina nyingine mbadala
Dawa ambazo ni mwiko kutumika pamoja na ALU
Dawa ambazo hazipaswi kutumika na ALU ni
Arsenic trioxide
Bosentan
Carbamazepine
Chloroquine
Clomipramine
Dexamethasone
Disopyramide
Enzalutamide
Eslicarbazepine acetate
Etravirine
Fluoxetine
Fosphenytoin
Goserelin
Ibutilide
Indapamide
Leuprolide
Mizizi ya st john's
Nevirapine
Oxcarbazepine
Pentamidine
Pentobarbital
Phenobarbital
Phenytoin
Pimozide
Primidone
Procainamide
Quinidine
Rifabutin
Rifampin
Rifapentine
Sotalol
Dawa ambazo zinaleta madhara zikitumika na ALU
Dawa ambazo zinaweza kuleta madhara makubwa endapo zitatumika na ALU
Abametapir
Amiodarone
Amitriptyline
Amoxapine
Apalutamide
Carvedilol
Chlorpromazine
Cimetidine
Clarithromycin
Clomipramine
Dabrafenib
Dapsone topical
Deflazacort
Desipramine
Dihydroergotamine
Dihydroergotamine ya puani
Dofetilide
Doxepin
Dronedarone
Droperidol
Duloxetine
Efavirenz
Epinephrine
Epinephrine racemic
Ergotamine
Eribulin
Erythromycin base
Erythromycin ethylsuccinate
Erythromycin lactobionate
Erythromycin stearate
Escitalopram
Everolimus
Flecainide
Fluconazole
Fluphenazine
Formoterol
Glasdegib
Haloperidol
Histrelin
Hydroxychloroquine sulfate
Idelalisib
Iloperidone
Imipramine
Inotuzumab
Ivosidenib
Ketoconazole
Lofepramine
Lovastatin
Macimorelin
Maprotiline
Methamphetamine
Metoprolol
Mexiletine
Mifepristone
Morphine
Moxifloxacin
Nebivolol
Nefazodone
Nilotinib
Nortriptyline
Octreotide
Octreotide (antidote)
Ondansetron
Oxycodone
Oxymorphone
Panobinostat
Perphenazine
Pimavanserin
Prochlorperazine
Promazine
Promethazine
Propafenone
Propranolol
Protriptyline
Ranolazine
Ribociclib
Romidepsin
Saquinavir
Silodosin
Simvastatin
Sirolimus
Thioridazine
Timolol
Tolvaptan
Trazodone
Trifluoperazine
Trimipramine
Triptorelin
Umeclidinium bromide/vilanterol kuvuta kwa pumzi
Vandetanib
Vemurafenib
Vilanterol/fluticasone furoate ya kuvuta kwa pumzi
Ziprasidone
Matumizi ya ALU na chakula na baada ya kutapika
Inashauriwa kunywa ALU baada ya kula chakula
Kwa watoto dawa inaweza kupasuliwa na kulainishwa kabla ya kunywa au kuchanganya kweye uji
Pia inaweza kuchanganywa ikaliwa kenye chakual
Endapo utatapika dozi ya ALU ufanyaje?
Endapo utatapika ALU ndani ya saa 1 hadi 2 baada ya kunywa, unapaswa kunywa dozi nyingine
Maudhi ya ALU.
Maudhi ya dawa
Maumivu ya tumbo
Kukosa hamu ya kula
Maumivu ya maungio
Kutetemeka
Kizunguzungu
Uchovu mkali
Asthenia (38%)
Maumivu ya kichwa
Maumivu ya misuli
Kichefuchefu
Hisia za mapigo ya moyo
Kuongezeka kwa joto la mwili
Madhaifu ya kulala
Kutapika
Maudhi ambayo yanatokea kidogo;
Kikohozi
Kuharisha
Kuvimba kwa ini
Uchovu kiasi
Koo kuuma
Muwasho
Harara
Kuvimba kwa bandama
Kizunguzungu
Matumizi ya ALU kwenye ujauzito
Tafiti za matumizi ya ALU wakati wa ujauzito hazijaonyesha mahusiano ya matumizi ya ALU na kusababisha ulemavu mkubwa wa kuzaliwa, kutoka kwa mimba au madhara kwa mama na mtoto hata baada ya kuzaliwa.
Matumizi ya ALU kwa mama anayenyonyesha
Hakuna taarifa zinazozungumzia kwamba dawa hii inaingia kwenye maziwa ya mama wakati wa ujauzito, na kama kuna madhara yoyote kwa mtoto anayenyonya maziwa ya mama. Hata hivyo tafiti zinaonyesha kuwa maziwa dawa huingia kwenye maziwa ya panya na hivyo kwa binadamu pia inaingia. Endapo kuna uhaja wa kunyonyesha wakati mama anatumia dawa hii, faida za kunyonyesha ziwe kubwa kuliko madhara yanayoweza kujitokeza Soma zaidi kuhusu ALU na ujauzito na kunyonyesha kwenye Makala nyingine ya matumizi ya dawa wakati wa ujauzito na kunyonyesha.
Endapo umesahau dozi ya ALU ufanyaje?
Endapo umesahau kunywa dozi yako ya ALu, kunywa mara pale utakapokumbuka isipokuwa endapo muda wa dozi ningine umekaribia sana. Endapo muda wa dozi nyingine umekaribia sana, acha dozi uliyosahau na endelea na dozi inayofuata kama ulivypangiwa na daktari wako
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:56
Rejea za mada hii:-