Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
21 Agosti 2021, 16:48:06

Ampicillin
Penicillin ni kundi la kwanza la antibayotiki lenye uwezo wa kukabiliana na bakteria wa Gram hasi, bakteria ambayo hawatoi kimeng’enya cha Beta Lactam.
Dawa zilizo kundi moja na Amoxicillin
Amoxicillin
Bacampicillin
Penicillin G
Penicillin V
Methicillin
Piperacillin
Procaine Penicillin
Dicloxacillin
Ampicillin hutibu nini?
Hutibu maambukizi ya bakteria kwenye, masikio na koo
Hutibu Maambukizi katika mfumo wa mkojo
Hutibu maambukizi katika mfumo wa umeng’enyaji chakula
Hutumika kwa ajili kukinga maambukizi ya bakteria kwenye misuli ya ndani ya moyo (endocarditis)
Hutibu kaswende
Hutibu homa ya uti wa mgongo
Namna Ampicillin inavyoweza kufanya kazi
Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia ukuajia wa Bakteria ndani ya seli yake ambapo huzuia hatua ya mwisho ya utengenezaji wa ukuta wa seli.
Ufyozwaji wa Ampicillin
Dawa hii hufyonzwa vizuri inapoingia kwenye mfumo wa chakula
Vimelea wanaodhuriwa na Ampicillin
Escherichia Coli
Haemophilus influenza
Streptococci
Neisseria Gonorrhoea
Baadhi ya makundi ya Staphylococcus
Helicobacter pylori
Mwingiliano wa Ampicillin na chakula
Ampicillin ni nzuri endapo itatumika pamoja na chakula ,Kwani chakula huongeza ufyonzwaji wa dawa hii vizuri
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Ampicillin
Wagonjwa wenye mzio na dawa jamii ya Penicillin
Wagonjwa wenye mzio na dawa jamii ya cephalosporins
Utoaji taka wa Ampicillin mwilini
Asilimia 85 ya dawa hutolewa kwa njia ya mkojo na asilimia zinazobaki hutolewa kwa njia ya haja kubwa
Matumizi ya Ampicillin kwa mama mjamzito
Kufahamu kuhusu ushauri wa matumizi ya Ampicillin wakati wa ujauzito bofya linki inayofuata https://www.ulyclinic.com/madhara-ya-dawa-kwa-mjamzito-na-mto
Matumizi ya Ampicillin kwa mama anayenyonyesha
Dawa hii huweza ingia kwenye maziwa ya mama na hivyo kama itatumika tahadhali inapaswa kuchukuliwa
Dawa zenye mwingiliano na Ampicillin
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa tumika kwa pamoja na Ampicillin ni
Chanjo ya BCG kwa watoto
Doxycycline
Tetracycline
Demeclocycline
Oxytetracycline
Sarecycline
Eravacycline
Omadacycline
Ampicillin ikitumika na dawa zifuatazo mgonjwa anapaswa kuwa chini ya ungalizi wa karibu na mtaalamu wa afya;
Aspirin
Aspirin/citric acid/sodium bicarbonate
Bazedoxifene/conjugated estrogens
Chloroquine
Choline magnesium trisalicylate
Deflazacort
Dexlansoprazole
Dienogest/estradiol valerate
Esomeprazole
Ethinylestradiol
Ibuprofen/famotidine
Lansoprazole
Lanthanum carbonate
Levonorgestrel oral/ethinylestradiol/ferrous bisglycinate
Mestranol
Methotrexate
Omeprazole
Pantoprazole
Sodium bicarbonate
Spironolactone
Sulfasalazine
Warfarin
Dawa zenye mwingiliano mdogo na Ampicillin
Allopurinol
Atenolol
Azithromycin
Bendroflumethiazide
Chloramphenicol
Chlorothiazide
Clarithromycin
Colestipol
Didanosine
Erythromycin base
Erythromycin ethylsuccinate
Erythromycin lactobionate
Erythromycin stearate
Hydrochlorothiazide
Methyclothiazide
Metolazone
Rifampin
Roxithromycin
Maudhi madogo ya Ampicillin
Kizunguzungu
Kiungulia
Kukosa usingizi
Kichefuchefu
Kuwashwa mwili
Kutapika
Maumivu ya tumbo
Mzio
Kichwa kuuma
Kuishiwa damu
Kuhara
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje ?
Kama umesahau kutumia dozi yako dozi yako, unaweza (tumia) mara pale utakapokumbuka ,isipokuwa kama muda wa dozi nyingine umekaribia sana unatakiwa kuruka dozi uliyosahau na kuendelea inayofuata kama muda uliopangiwa na daktari wako
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:56
Rejea za mada hii:-