top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

23 Aprili 2020 11:39:19

Azathioprine

Azathioprine

Azathioprine ni dawa jamii ya imyunosaprizanti inayofanya kazi ya kupunguza mwitikio wa mfumo wa kinga dhidi ya maradhi. Dawa hii hutumika pamoja na dawa zingine ili kuzuia mwili kukataa figo ya kupandikiza ili ifanye kazi vizuri. Hupatikana mfumo wa kidonge chenye milligramu 50.


Kazi za dawa


  • Kuzuia uharibifu wa maungio (joint) hutibu baridi yabisi

  • Kuzuia mwili kukataa figo ya kupandikiza

  • Kutibu ugonjwa wa inflamatori bawel na sistemiki lupasi erithromatosasi


Jinsi inavyofanya kazi

Haieleweki vema ni namna gani dawa hii inafanya kazi yake ya kupunguza mfumo wa kinga. Baadhi ya tafiti za kisayansi zinaonyesha kuwa dawa hii huanzisha uuaji wa seli za ulizi zinazofahamika kwa jina la seli T na kuzuia uzalishaji wa seli B na T pamoja nap rotini muhimu za pyurini zinazohusika kutengeneza msingi wa jinomu.


Maudhi madogo madogo ya dawa ni


  • Kichefuchefu na kutapika

  • Kupata maambukizi

  • Kupoteza hamu ya kula

  • Kuharisha

  • Uchovu wa mwili

  • Upele wa ngozi

  • Maumivu ya tumbo

  • Kupumua kwa shida

  • Maumivu ya misuli


Angalizo

Tumia dawa hii kwa Umakini kwa watu wafuatao


  • Wenye shida ya Figo au kuwa na historia ya kupandikiziwa Figo

  • Wenye shida ya Ini

  • Wenye kansa

  • Wenye aleji au mzio na dawa hii au aleji nyingine

Usitumie dawa hii pamoja na dawa zifuatazo


  • Usitumie dawa hii pamoja na dawa Allopurinol

  • Usitumie dawa hii pamoja na dawa febuxostat

  • Usitumie dawa hii pamoja na dawa Ribavirin

  • Usitumie dawa hii pamoja na dawa za kansa mfano melphalan, cyclophosphamide

  • Usitumie dawa hii pamoja na dawa nyinginezo zinaathiri kinga ya mwili mfano rituximab, tofacitinib


Dawa zinazo athiri mfumo wa kinga ya mwili zinaweza kuongeza hatari ya maambukizi. Hivyo tahadhari kuchukuliwa.


Kwa Wajawazito

Tahadhari wakati wa ujauzito isitumike kwa mama mjamzito haswa miezi mitatu ya mwanzoni na miezi ya mitatu mwishoni ya ujauzito.


Kwa Wanaonyonyesha


Dawa hii isitumike kwa mama anaenyonyesha. Sababu dawa hii hupita katika maziwa ya mama na hivyo kuleta athari kwa mtoto anaenyonyesha.

Kundi la dawa wakati wa ujauzito


Dawa ipo kwenye kundi D la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito. Tafiti zinaonyesha kuwa dawa hii ikitumika wakati wa ujauzito huleta madhata makubwa kwa mtoto ambao ni kuwa na vidole vingi Zaidi ya kawaida- polidaktili, plagiosefali, magonjwa ya moyo ya kuzaliwa, haipospadiasis na mguu kifundo. Leukopenia na thrombosaitopenia.

Ukisaau dose Nini kifanyike

Kama umesaau kunywa dose yako Unaweza kunywa Mara tu unapokumbuka Isipokua endapo muda wa dozi nyingine umefika Unatakiwa kuruka hiyo dozi uliyosaau na kuendelea na dozi yako kwa muda uliopangiwa. Usitumie dozi mbili kwa wakati mmoja.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021 11:49:52

Rejea za mada hii:-

1.Azathioprine Uses, side effects, warnings. https://www.drugs.com/mtm/azathioprine.html. Imechukuliwa 22.4.2020

2.Azathioprine Uses, side effects, interactions. https://www.webmd.com/drugs/2/drug-13771/azathioprine-oral/details. Imechukuliwa 22.4.2020

3.Azathioprine Uses, side effects, dosage, Interactions. https://www.rxlist.com/imuran-drug.htm. Imechukuliwa 22.4.2020

4.Azathioprine. https://www.drugbank.ca/drugs/DB00993. Imechukuliwa 22.4.2020

5.Drugs.com. azathioprine. https://www.drugs.com/pregnancy/azathioprine.html. Imechukuliwa 22.4.2020
bottom of page