Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
20 Aprili 2020 12:40:36
Bendroflumethiazide
Bendroflumethiazide ni aina ya dawa iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa Thayazaidi Dyuretiksi, dawa hii huuzwa katika jina la Aprinox na hupatikana katika mfumo wa kidonge. Hutumika kutibu shinikizo la juu la damu na mwili kujaa maji.
Rangi ya dawa
Mara nyingi huwa nyeupe na kidonge huwa na uzito wa miligramu 5.
Dawa hii haina madhara inapotumika pamoja na chakula na haishauriwi kutumika ukiwa unakaribia kulala kwa sababu itakubidi kuamka mara kwa mara ili kukojoa nyakazi za usiku haswa masaa mawili baada ya kunwywa dawa.
Dawa hii ipo kwenye kundi sawa na dawa zifuatavyo;
Hydrochlorothiazide
Chlorothiazide
Methyclothiazide
Polythiazide
Indapamide
Metolazone
Dawa hii imeonekana kuzuia madhara yanayoweza kutokana na shinikizo la juu la damu hata hivyo namna inavyoweza kuzuia madhara hayo haifahamiki bado.
Kazi za Bendroflumethiazide kama zifuatavyo:
Hutumika kutibu uvimbe wa mwili kutokanana kutuwama kwa maji mfano kuvimba miguu na uso hali hii huweza kuwatokea kwa wagonjwa wa moyo ulioferi kwa kujawa maji na wagonjwa wa ini na figo
Hutumika kutibu ugonjwa wa shinikizo la juu la damu
Dozi na uzito wa Bendroflumethiazide
Dawa hii hutolewa kwa dozi ya Mg 5 kwa siku lakini hata hivyo dozi hutegemea umri na afya ya mtu.
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:
Allupurinol
Colestyramine
Colestipol
Disopyramide
Amiodarone
Flecainide
Quinidine
Glibenclamide
Carbamazepine
Amphotericin
Pimozide
Digoxin
Lithium
Tizanidine
Tahadhari ya dawa hii;
Huweza kupandisha kiasi cha uric asidi kwa wingi kwenye damu
Hupaswa kutumika kwa Tahadhari kwa wagonjwa wa figo na ini
Haipaswi kutumika kwa wagonjwa wenye;
Mzio na dawa hii
Matatizo ya ini na figo
Wenye madini ya kalisiamu kwa wingi (haipakalemia)
Wenye upungufu wa madini ya sodiamu kwenye damu(haipokalemia)
Wenye ugonjwa wa addison
Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Dawa hii haipaswi kutumika kwa mama mjamzito Pamoja na mama anayenyonyesha.
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa ni;
Kukojoa mara kwa mara
Kushuka kwa shinikizo la damu (haipotensheni)
Kuhara au choo kuwa kigumu
Kuchoka
Maumivu ya tumbo
Kushuka kwa kiasi cha madini ya Sodiamu, potasiumu na magneziamu kwenye damu.
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo mgonjwa atasahau kutumia hii dawa anapaswa kutumia pindi anapokumbuka. Isipokuwa endapo muda wa dozi ingine umefika, acha dozi uliyosahau endelea na dozi nyingine kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:50:19
Rejea za mada hii:-