Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
27 Mei 2020, 09:21:41
Betaxolol
Betaxolol Ni aina ya dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa beta bloka. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Kerlone.
Rangi ya dawa
Rangi yakeya kidonge huwa ni nyeupe japo mara nyingi utegemea aina ya kiwanda kinachotenegeneza
Betaxolol hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa;
10mg
20mg
Namna dawa inavyofanya kazi kupunguza shinikizo la damu.
Dawa jamii ya beta bloka ikiwemo betaxolol hufanya kazi zifuatvyo ili kupunguza shinikizo la damu;
Hufanya kazi kwa kuzuia matendo yanayosababisha mapigo ya moyo kwenda kasi kwa kupinga utendji kazi wa seli za beta adrenorisepta.
Matendo ya carvediolol kwenye seli za alfa 1 adrenejik risepta hufanya misuli ya damu kulainika, hivyo hupelekea kupungua kwa upinzani wa mzunguko wa damu ndani ya mishipa ya damu. Matendo haya hupelekea kupungua kwa shinikizo la damu na hivyo kuruhusu mzunguko wa damu kuwa mzuri mwilini.
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo:
Atenolol (Tenormin)
Betaxolol (Monocor,Zebeta)
Acebutolol (Sectral )
Carteolol (Cartrol)
Carvedilol (Coreg)
Labetalol (Normodyne, Trandate)
Metoprolol (Lopressor, Toprol-XL)
Nadolol (Corgard)
Nebivolol (Bystolic)
Penbutolol (Levatol)
Pindolol (Visken)
Propanolol (Inderal)
Sotalol (Betapace)
Timolol (Blocadren)
Kazi za hii dawa ni kama ifuatavyo:
Hutumika kushusha shinikizo la damu kwa wagonjwa wenye shinikizo la damu la juu
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:
Acebutolol
Betaxolol
Bisoprolol
Carvedilol
Celiprolol
Clonidine
Digoxin
Diltiazem
Esmolol
Labetalol
Lofexidine
Metoprolol
Nadolol
Nebivolol
Penbutolol
Pindolol
Propranolol
Rivastigmine
Saquinavir
Sotalol
Timolol
Verapamil
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au dawa zingine jamii ya Beta bloka
Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye kisukari
Wagonjwa wenye haipathairodizim
Wagonjwa wenye shida ya figo
Wagonjwa wenye shida ya Ini
Wagonjwa wenye shida ya Moyo kuferi
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la (beta bloka):
Nusu ya maisha ya dawa hii huchukua masaa 14 mpaka 22 baada ya kutumiwa
Matumizi kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Dawa hii itumike kwa tahadhari kwa mama mjamzito.
Dawa hii inauwezakano wa kuwa kwenye maziwa hivyo itumike kwa uangalifu kwa mama anayenyonyesha
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na;
Mwili kuchoka
Maumivu ya kifua
Kuharisha
Edima
Kutokwa na vipele
Haipoglaisemia
Dayabeti
Miguu kuwa ya baridi
Kukohoa
Anjaina
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kunywa dozi yako, kunywa mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:55:55
Rejea za mada hii:-